Kiongozi wa kisiasa wa M23, Mr. Bisimwa akizungumza na wakazi wa North Kivu.
Kwa mujibu wa mwandishi aliye na waasi wa m23, Diana Katabarwa kwenye Blog yake anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23 Mr. Bisimwa akiwambia wakazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo....
Bisimwa anadai kwamba majeshi ya Tanzania yamekuja kuiba mali na kumsaidia KABILA awatawale hali itakayosababisha jeshi lake la FDLR na waasi wa MAI MAI wapewa nafasi ya kuwa pora mali zao na kuwabaka wake zao na watoto....
Mbali na hayo, bwana Busimwa anadai kinyume na taarifa zilivyo , kikosi cha jeshi la Tanzania kikiwa na askari 450 kimesha ingia mashariki ya CONGO kwenye mji wa UVIRA SOUTH KIVU huku Kamanda wao (TPDF) akiwa mjini Goma.
Kikosi cha jeshi la SOUTH AFRICA kiko mita 20 kutoka waasi walipo kwenye mji wa MUNGI nje kidogo ya GOMA.
Pia aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna makomandoo 30 wa jeshi la Ufaransa ambao wako mjini GOMA na wamefikia Linda Hotel...
BUSIMWA alidai wafaransa ndio walisimamia mauaji ya kimbari ya Rwanda ,kwa hiyo kuwepo kwao ni ishara mbaya kwa wakazi wa mashariki ya CONGO ambao wengi ni watusi.
No comments:
Post a Comment