Mwnyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe |
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman ameweka bayana kuwa
wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania
kuundwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa kazi
na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu
hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania
Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani wa Kata ya Iyela
katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe alisema chama chake
kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi
mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili
wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini
waunganishwe na Serikali ya Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano, mbunge wa
Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa
Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano
utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi
kidogo yatakoma.”
Msimamo wa Sumaye
Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.
Sumaye anaungana na wanasiasa wengine waliopinga muundo wa Serikali
tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wengine wakiwa ni
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene, Mbunge wa Urambo Magharibi
(CCM) Profesa Juma Kapuya, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba
na Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Daftari.
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dira ya Dunia
kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiwa
Johannesburg, Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, alisema Serikali tatu
zinaweza kutikisa Muungano.
“Huwezi kutatua matatizo kwa Serikali tatu… unaweza kuyaongeza kwani
kutakuwa na Serikali tatu na marais watatu… kama kuna mvutano baina ya
Serikali mbili ukiongeza ya tatu inaweza kuwa na mvutano zaidi,” alisema
na kuongeza:
Lipumba: Katiba ya Bara kwanza
Profesa Lipumba alisema hakuna mantiki ya kupiga kura ya maoni ya
Katiba ya Muungano bila kuwa na Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho
ya Katiba ya Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa
Lipumba alisema mapendekezo ya msingi ya CUF ni kwamba, kura ya maoni
isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya Katiba ya Tanzania Bara na
marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Alisema licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya kazi nzuri ya
kuratibu maoni bila kushinikizwa na matakwa ya CCM, kuna baadhi ya mambo
ya msingi ambayo yameachwa kwenye rasimu.
“Huwezi kuacha vitu kama umilikaji wa ardhi, maliasili na rasilimali
za nchi, elimu, afya na mazingira ya kukuza uchumi na uhuru wa Serikali
za mitaa. Rasimu imeshughulikia mambo ya Muungano.”
“Maoni ambayo CUF tuliyatoa ikiwamo muundo wa Serikali tatu,
kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, Rais kutangazwa baada ya kushinda kwa
zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, Spika kutokuwa mbunge na mengineyo
yamepata nafasi.”
CHANZO: mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment