Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, June 29, 2013

KNCU WAPO MBIONI KUFUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA VIPIMO MAALUMU...!

Picture
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro (KNCU) Menard Swai akitoa taarifa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika katika ukumbi wa Hotel ya KNCU uliopo mjini Moshi.
CHAMA Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) kipo mbioni kuanzisha hospitali ya rufaa ya vipimo maalumu, kwa lengo la kuisaidia jamii ambayo wengi ni wakulima kwa lengo la kuepuka gharama za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa chama cha KNCU, Menard Swai, wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho kwenye mkutano mkuu, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya KNCU iliyopo mjini Moshi mkoani hapa.

Swai alisema uongozi wa bodi upo kwenye mchakato wa kuandaa andiko la kupata wafadhili ambao wanaweza kusaidia mchakato huo, kwa lengo la kuboresha afya za wakulima na kuokoa gharama kubwa za matibabu, kulingana na ugonjwa husika.

“Tunafanya mchakato mkubwa wa kuhakikisha tunakuwa na hospitali ya kisasa ya rufaa kwa ajili ya vipimo peke yake, hii ni maalumu zaidi kwa wakulima kwani itawasaidia kupata vipimo mbalimbali vya mwili kwa lengo la kujua hali ya afya zao,” alisema Swai.

Alisema lengo maalumu la kuanzisha mchakato huo ni kuokoa pia vifo visivyotarajiwa, vinavyotokana na ukosefu wa wakulima kutopata vipimo vya mara kwa mara vya kutambua afya zao, kutokana na sumu zitokanazo na madawa yanayotumika kwenye kilimo cha kahawa.
Picture
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KNCU wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwenyekiti.

Source: wavuti.com

No comments:

Post a Comment