BAADA ya kuchaguliwa katika awamu ya pili ya utawala wa
Marekani, Rais Barack Obama, ameendelea kupata mshahara wa dola 400,000
kwa mwaka.
Wakati alipopata utawala, Rais huyo mwenye nguvu
duniani ameendelea kuwa Kamanda wa Jeshi la Marekani, Rais mwenye nguvu
duniani na ameendeleza utawala wa Air Force One.
Obama alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza, kipato
chake kilikuwa dola 1.3 milioni. Miaka minne baada ya kukaa Ikulu kipato
chake kimeongezeka kwa asilimia 800 sasa anapata dola 11.8 milioni.
Kipato kimeongezeka vipi?
Awali Obama alikuwa na kipato kidogo, alikuwa
akilipwa dola 60,000 kwa mwaka alipokuwa Seneta wa Illinois na baadaye
akawa analipwa dola 175,000 kwa mwaka.
Jambo la kufurahisha ni kuwa kabla Obama hajawa
Rais, hakuwa na mshahara mkubwa, hata mke wake, Michelle, alimzidi kwa
kipato. Michelle alikuwa akiingiza kiasi cha dola 320,000 kwa mwaka,
wakati huo alikuwa Makamu wa Rais wa Kitengo cha Ushirikiano wa Jamii
katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Chicago.
Lakini Michelle alipitwa mshahara na mume wake wakati Obama alipounasa urais.
Kipato cha Obama kilianza kukua baada ya kujiimarisha kwenye Chama cha Democratic mwaka 2004.
Vile vile jina la Obama lilikua baada ya kuuza kitabu chake alichokiandaa tangu mwaka 1995 kiitwacho ‘Dreams From My Father’.
Mwaka 2005, kipato cha Obama kiliongezeka kufikia
dola 200,000 na hivyo akatimiza dola 1.7 milioni kwa mwaka. Mwaka 2006
kipato cha Obama kilikua na kufikia dola 916,000.
Kitabu cha pili cha Obama kiitwacho ‘Audacity of
Hope’ kilitolewa Oktoba, 2006 na kiliongoza kwa mauzo makubwa kiasi cha
kumfanya Obama apate dola 4.2 milioni mpaka kufikia mwaka 2007.
Mpaka sasa Obama amekuwa akipata dola 3.75 milioni kutokana na
kuuza vitabu vyenye gamba gumu na dola 1.12 milioni kutokana na kuuza
vitabu vyenye gamba la kawaida.
Kwa kuwa Obama haruhusiwi kutoa vitabu kuhusu
maisha yake ya urais kwa sasa, watu wanasubiri wakati atakapomaliza
utawala wake mwaka 2016 ambapo atatoa vitabu vingi zaidi.
Rais George W. Bush, aliwahi kuingiza dola 7
milioni kwa kuandika kitabu cha ‘Decision Points’ na Bill Clinton
alipata dola 15 milioni kwa kuandika kitabu cha ‘My Life’.
Lakini ukweli ni kwamba Clinton aliuza vitabu
vichache kuliko Bush, kitu kilichomsaidia kupata fedha nyingi ni bei
kubwa ya vitabu vyake.
Inakadiriwa kuwa Obama atakuwa amejikusanyia kiasi
cha dola milioni 100 au zaidi wakati atakapostaafu kazi. Huenda
akafuata nyayo za Bill Clinton ambaye alimaliza utawala wake akiwa na
utajiri wa dola 80 milioni.
Historia ya kipato cha familia ya Obama
2000: Dola 240,000
2001: Dola 272,759
2002: Dola 259,394
2003: Dola 238,327
Historia
2005: Dola 1,655,106
2006: Dola 983,826
2007: Dola 4,139,965
2008: Dola 2,656,902
2009: Dola 5,505,409
2010: Dola 1,728,096
2011: Dola 789,674
Jumla: Dola 18,563,000
Historia
Barack Obama ambaye ni rais wa 44 wa Marekani,
alizaliwa Honolulu, Hawaii. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Columbia na
Chuo Kikuu cha Sheria cha Harvard.
Wakati akisoma sheria, alikuwa pia akifanya kazi
za maendeleo ya jamii huko Chicago. Baada ya kumaliza masomo hayo
alifanya kazi katika Kitengo cha Haki za Raia huko Chicago na kuanzia
1992 mpaka 2004 alifundisha Sheria ya Katiba katika Chuo Kikuu cha
Chicago.
Obama alianza kuonekana mbele za watu wakati
alipojiimarisha kwenye Chama cha Democratic mwaka 2004. Novemba 2008
alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani na Januari 2009 aliingia Ikulu.
Obama ni mume wa Michelle, baba wa watoto wawili wa kike, Malia Ann aliyezaliwa mwaka 1998 na Natasha ‘Sasha’ aliyezaliwa mwaka 2001.
Obama ni mume wa Michelle, baba wa watoto wawili wa kike, Malia Ann aliyezaliwa mwaka 1998 na Natasha ‘Sasha’ aliyezaliwa mwaka 2001.
No comments:
Post a Comment