MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC) JIJINI MBEYA
KATIBU TAWALA WA MKOA MARIAM MUTUNGUJA AKISOMA TAARIFA YA MKUTANO
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO
MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MBEYA GODFREY ZAMBI AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO HICHO
MKUU WA WILAYA WA MBEYA DR. NORMAN SIGARA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO
MBUNGE WA VITI MAALUMU(CCM) MKOA WA MBEYA DR. MARY MWANJELWA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO.
MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS kAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPIN MEELA AKIZUNGUMZA JAMBO
WAJUMBE WAKIWA WANAFUATILIA MKUTANO HUO
Songwe
ndilo jina lililopendekezwa kuwa la Mkoa Mpya utakaogawanywa kutoka
Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba
ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.
Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za
Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.
Kupatikana
kwa jina hilo na mwafaka huo kumetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri
ya Mkoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa
na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na
Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao unapita katika Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.
Hata
hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa
mapendekezo hayo ya RCC.
No comments:
Post a Comment