Elizabeth Michael maarufu kwenye bongomovie kama Lulu na maarufu kwenye
mitandao ya kijamii kama hotlulumichael, hivi karibuni nyota yake
imeendelea kung’aa tena kwenye tamasha kubwa la filamu africa. Kupitia
category ya “Best Actress Swahili Movies” ambayo ilikuwa na ushindani
mkubwa kutokana na uwepo wa wasanii wengi wa kike wanaofanya vizuri kwa
sasa, lakini Elizabeth Michael a.k.a Lulu amenyakuwa tuzo hii kwenye
tamasha la ZIFF ambalo ni maarufu na linahudhuriwa na wadau mbalimbali
wa filamu kutoka sehemu tofauti duniani. Hivyo basi hii itakuwa ni fursa
nyingine na nzuri kwa Lulu baaada ya wadau wa movie kumjua yeye na
labda kufuatilia kazi zake kitu ambacho kinaweza kumsaidia kufika zaidi
ya hapa alipo sasa kwa kupata kazi nyingine nje ya Tanzania. Lulu
ameshinda tuzo hii kutokana na ushiriki wake kwenye movie ya Woman of
principle. Movie hii iliandaliwa na kampuni ya RJ Company na kufanywa na
Ray,Lulu na Nagris Mohamed kama washiriki wakuu.
No comments:
Post a Comment