RAis Obama Akiagana na Raisi wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania J.Kikwete |
Rais Obama akiwaaga watanzania waliofika katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Rais wa Marekani Barack Obama ameondoka nchini muda huu kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa M Julius Nyerere huku maelfu ya wananchi wa Tanzania wakijitokeza barabarani kumuaga.
Rais Obama alikuwa nchini katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapoametaja
vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania, ambavyo vinajumuisha miradi
mbalimbali ya umeme, miundombinu ya barabara, maji na programu za
kielimu kwa vijana kwa lengo la kuongeza ajira
Jijini Dar es salama Barabara za Ally Hassan
Mwinyi, Mandela, Sam Nujoma na ile ya Morogoro zilifungwa kwa muda
kuanzia majira ya saa tatu asubuhi huku maelfu ya wananchi wakitanda
barabarani kwa lengo la kumuaga rais huyo.
Mara baada ya kufika katika uwanja wa Ndege Rais
Obama na Mkewe walitumia muda mfupi kuagana na mwenyeji wao Rais
Kikwete na mkewe ikiwa ni pamoja na kuwaaga mamia ya viongozi waliofika
uwanjani hapo.
fuatana nasi kwa taarifa zaidi
Rais Obama awasili, aisifu Tanzania
Dar es Salaam. Rais Barack wa
Marekani, Obama ametaja vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania,
ambavyo vinajumuisha miradi mbalimbali ya umeme, miundombinu ya
barabara, maji na programu za vijana kwa lengo la kuongeza ajira.
Kiongozi huyo aliwasili Dar es Salaam jana mchana
ikiwa ni nchi ya mwisho katika ziara yake barani Afrika ikitanguliwa na
Senegal na Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais
Jakaya Kikwete Ikulu, Rais Obama alisema aliainisha mambo hayo wakati
alipozungumza na mwenyeji wake huyo.
Alisema katika mazungumzo hayo, waligusia mradi wa
mkubwa wa umeme uitwao Power Afrika wenye lengo la kuongeza kiwango cha
umeme kinachozalishwa nchini na barani Afrika ili kupata umeme nafuu na
wa uhakika utakaochagiza kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.
Nchi nyingine za Afrika ambazo zitanufaika na mpango huo ni Kenya, Ghana, Liberia, Nigeria na Ethiopia.
Rais Obama alisema pia wamezungumzia masuala
mbalimbali ya maendeleo, ukuzaji wa demokrasia na utawala bora.
Alimzungumzia pia mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hashimu
Thabeet anayecheza katika Ligi Kuu ya Marekani (NBA), akiwa na timu ya
Oklahoma Thunder ya Marekani, akisema hawakuzungumzia suala lake na
kuahidi kufanya hivyo siku nyingine.
No comments:
Post a Comment