MOSHI meya wa manispaa ya
Moshi mkoani Kilimanjaro, Jaffari Michael, ameelezea kusikitishwa kwake na
tabia ya maamuzi yanayopitishwa na halmashuari hiyo kutokutekelezwa na
wahusishwa.
Michael alielezea
kusikitishwa kwake huo wakati wa baraza la halmashuari hiyo lililokaa ambapo
ilibidi kubadilishwa kuwa kamati, baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kutaka
iwe hivyo ili kuwawajibisha watendaji wababaishaji katika kutekeleza maamuzi ya
baraza la madiwani.
Alisema jambo hilo
linazidi kuweka mashaka dhidi ya watendaji mbalimbali wa halmashauri hiyo ya
kuwa wamebobea katika rushwa na kwamba katika siku za hivi karibuni, maeneo ya
wazi yamekuwa yakilengwa na watendaji ambao si waaminifu kwa kuwagawia watu kwa
misingi ya rushwa.
Akichangia hoja hiyo,
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaban Ntarambe, alitoa rai kwa madiwani kuachana na wazo la kuligeuza baraza
hilo kuwa kamati maalum kwa madai kuwa si rahisi kuigeuzwa kuwa hiyvo.
Pamoja rai hiyo, madiwani
hao waliisimamia hoja yao ya kuligeuza baraza hilo kuwa kamati maalum baada ya
meya Michael kuagiza kura zipigwe.
Madiwani hao walifikia
uamuzi huo kufuatia malalamiko yaliyojitokeza kufuatia mtu mmoja kujenga eneo
la wazi pamoja na halmashuari hiyo kuagiza litumiwe kujenga ofisi ya kata.
Madiwani hao walidai
kuwa mara baada ya kuona kuwa eneo hilo limevamiwa na kuwekwa vifaa vya ujenzi
ikiwemo mchanga, walitoa maamuzi ya kutaka vitu hivyo viondolewe bila mafanikio
na badala yake ujenzi wa eneo hilo ulionekana kuendelea kujengwa ambapo pamoja
na maamuzi kutolewa pabomolewe amri hiyo bado haijatekelezwa.
No comments:
Post a Comment