SIHA imeelezwa kuwa baadhi ya wazazi kutokuchangia michango ya shule za msingi na
sekondari kwa wakati imekuwa ikichanguia
kushuka kwa kiwango cha elimu na
kusababisha uendeshaji wa shule kuwa mgumu
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya
Purming Godfrey Sauya wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo
katika maafali ya wanafunzi wa darasa la saba yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
Alisema baadhi ya wazazi wamekuwa
wakichangia zaidi kushindwa kufikia malengo ya shule kutokana na kushindwa
kulipa karo za wanafunzi kwa wakati jambo ambalo ni hatari katika kukuza elimu
hapa nchini
Aliwataka wazazi wa wanafunzi wanasoma shule mbalimbali hapa nchni
kuhahakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao wa kuwalipia wanafunzi wa michango ili
waweze kupatiwa elimu bora kutokana naa
fedha watakazochangia ambazo zitaweza kununua vifaa vya shule
Awali diwani wa Kata ya Karansi
Dancan Urassa alisema kuanzishwa kwa shule za msingi za watu binafsi zimechangia
zaidi kupunza mlundikano wa wanafunzi katika shule zinazomilikiwa na serikali jambo
ambalo limechangia zaidi kupunga watoto wenye umri wa kwenda shule kukosa
nafasi
Alisema jamii inatakiwa kuzitumia shule hizo kwani zimekuwa zikichangia
zaidi katika kuboresha elimu na kuwataka wananchi kuacha dhana ya kutochangia michango ya shule kwa
madai kuwa shule hizo zipo chini ya wahisani
Nae mkaguzi wa shule wa Wilaya hiyo Robatha Assey aliwataka
wazazi na walezi kupeleka watoto wao
katika shule hiyo ili waweze kupata
elimu na kuwawezesha kujiendeleza kutokana na elimu inayotolewa shule hapo.
Awali akisoma taarifa ya kituo
hicho, Mwanzilishi wa shule hiyo Mchungaji Wanaeli Mafie alisema shule hiyo wenye wafadhili kutoka kanisa la
Perimeta kutoka nchni Marekani ilianzishwa mwaka 2003 na tangu
kuanzishwa imekuwa ikifaulisha kwa asilimia moja
Alifafanua kuwa katika matokeo mtihani wa darasa la saba mwaka huu shule hiyo imeshika
nafasi ya pili kati ya shule 52 kiwilaya
na nafasi 30 kati ya 920 kimkoabaada ya kufaulisha wanafunzi wote walifanya
mtihani huo.
No comments:
Post a Comment