CHUO
Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) cha mkoani
Kilimanjaro, kimekabidhiwa majengo ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa
mkataba wa miaka mitano, lengo likiwa ni kuboresha maendeleo ya elimu
nchini Tanzania.
Hafla
ya makabidhiano hayo ilishuhudiwa na Meneja wa TBL Kanda ya Kaskazini,
Salvatory Rweyemamu na viongozi wengine wa chuo hicho, akiwemo Katibu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini,
Julius Mosi.
Akizungumza
baada ya kuingia mkataba huo, Rweyemamu alisema hatua hiyo inatokana na
kampuni hiyo kutambua umuhimu wa matumizi wa majengo hayo kwa chuo
hicho kwa maendeleo ya elimu nchini Tanzania.
Alisema TBL imeamua kuingia mkataba moja kwa moja na chuo hicho, ambao vilevile utahusisha punguzo la gharama za ukodishaji."Majengo
haya tumekuwa tukiyatumia kama stoo ya kuhifadhia bia, hata hivyo kwa
kutambua umuhimu wa matumizi ya majengo haya kwa uongozi wa chuo,
tunayakabidhi majengo haya tukiwa tumedhamiria kupunguza gharama za
ukodishaji pia," alisema Rweyemamu.
Alisema
awali majengo hayo, yalikuwa yakimilikiwa na Kampuni ya Kilimanjaro
Development Forum (KDF) na kwamba imeamua kuyakabidhi kwa chuo hicho
pamoja na kupunguza gharama za kuyakodisha kwa mwezi kutoka Sh milioni
8.4 hadi Sh 100,000 pamoja na kusimamia gharama nyinginezo kama vile
kodi ya viwanja.
"Tunafanya
hivi kama mchango wetu TBL katika maendeleo ya elimu hapa nchini,
lakini pia tunatarajia kusimamia gharama zozote zile, kama vile kodi ya
kiwanja," alisema Rweyemamu. Kwa
upande wake, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Julius Mosi, alisema
kitendo kilichooneshwa na TBL ni cha kiungwana, kizalendo na cha kuigwa
na makampuni mengine makubwa ambayo yanaingiza faida kubwa kutokana na
kodi za wananchi. Mkuu wa Chuo cha SMMUCo, Arnold Temu alisema chuo
hicho kina wanafunzi zaidi ya 2,603.
Alisema
kwamba kuongezeka kwa wanafunzi mwaka hadi mwaka tangu chuo kianzishwe
mwaka 2008, kumesababisha kuwe na haja ya kuongeza majengo.
No comments:
Post a Comment