Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Mkoani Kilimanjaro ndani ya Wilaya ya Mwanga ni chuo ambacho kilianzishwa mnamo mwaka 2006 ambacho kwa sasa kinazidi kukua kwa kasi kitaaluma huku kikiacha vyuo vingine vikongwe nyuma kitaaluma. Chuo cha Green bird ni chuo ambaho kinatoa Elimu katika Taaluma ya Biashara na Ualimu huku kikiwa na sifa ya Kutoa wahitimu ambao hupata ajira ya moja kwa moja kutokana na Ubora wa elimu ya Taaluma wanayoipata chuoni hapo.
Siku ya Jana ilikua siku ya Mahafali ya wahitimu wa Taaluma ya Ualimu na Biashara, Ambapo hapo jana Jumla ya Wahitimu 263 walitunukiwa yeti vya kuhitimu katika ngazi mbalimbali.
Chuo cha Green Bird ambacho kwa Mwaka Jana kimeweza kushika Namba Moja Tanzania nzima kwa kufaulisha kwa kiwango cha juu zaidi. Katika Mahafali hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Green Bird Ndugu. Juma H. Mndeme alitumia Fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuwa Watoto wao wanahitaji Elimu bora na Elimu bora hutolewa Sehemu iliyo Sahihi na si kwingine zaidi ya Chuo cha Green Bird.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kaluwa Development Trust Fund (KDTF) ndugu Juma H. Mndeme akifanya Utambulisho wa wageni Hapo jana katika Mahafali ya Chuo cha ualimu Green Bird.
Wahitimu wa Kozu ya Ualimu na Biashara wakimsikiliza Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi Muwakilishi ndugu Makyara Akimuwakilisha Mgeni Rasmi wa Mwanga akitoa Nasaha kwa Wahitimu
Mama Zuena Mndeme aliyekaa katikati ambae ni C.E.O wa Chuo Cha Green Bird Akimsikiliza Mgeni Rasmi kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa KDTF ndugu Juma H. Mndeme akitoa neno kwa Wahitimu.
Mkuu wa Chuo Bi Swaumu Alfan akifuatilia Hotuba ya Mkurugenzi wa Kaluwa Development Trust Fund kwa makini.
Uongozi na Walimu wa Chuo cha Green Bird wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment