Diwani wa kata ya Okaoni, Morisi Makoi alisema, alitoa taarifa kwa mkuu wa polisi wa wilaya, juu ya mwanafunzi huyo wa shule ya sekondari ya Okaoni (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 18, kutoweka nyumbani kwake na polisi huyo na taarifa zake zilienea zaidi baada ya ajali hiyo ya pikipiki.
Makoi ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi alisema, polisi huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la God, baada ya kufanya mapenzi walipata ajali na mwanafunzi huyo eneo la Memoria katika barabara kuu ya Moshi/Arusha akimrejesha kibosho.
Alisema, kitendo cha polisi huyo kinarudisha nyuma juhudi za serikali za kuwapatia elimu watoto wa kike na kueleza matumaini yake kuwa haki itapatikana kwa wakati na polisi huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu wa Kilimanjaro Official Blog, akiwa katika wodi namba tano mwanafunzi huyo alikiri kufanya mapenzi na polisi huyo baada ya kuahidiwa kununuliwa magauni mawili, blauzi mbili, sketi mbili ambazo baada ya ajali hajui ziko wapi na shs. 100,000/= ambazo hakupewa.
Mwanafunzi huyo alisema, baada ya kufika mjini Moshi alikwenda kununuliwa vitu hivyo na kwenda nyumba ya kufikia wageni ambako walifanya mapenzi na kwamba wakati wakirejea kibosho wakiwa na pikipiki hiyo walipata ajali eneo hilo na kukimbizwa katika hospital ya rufaa ya KCMC, iliyopo mjini Moshi.
Alisema walipata ajali hiyo saa tisa alasiri siku ya tarehe 27 septemba 2014, na kupoteza fahamu na saa sita za usiku alijikuta akiwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya kcmc na kesho yake alichukuliwa na polisi huyo kwa gari kurejeshwa nyumbani.
Mwanafunzi huyo alisema kuwa, baada ya kufika nyumbani maumivu yaliendelea kuwa makali na kuamua kupelekwa katika hospitali ya kibosho kuendelea na matibabu.
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Erin Massele alithibitisha kumpokea mwanafunzi hayo ambaye anaendelea vizuri akiwa na majeraha sehemu za miguu yote miwili na maumivu ya ndani ya mwili.
Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Moita Koka hakuweza kupatikana kuthibitisha juu ya tukio hilo ambalo lilishuhudia polisi huyo akiwa amebebwa kwenye kalandinga la jeshi hilo akipelekwa kituo kikuu cha polisi mjini Moshi.
Habari zilizopatikana jana kutoka kibosho zilieleza kuwa mwanafunzi huyo aliruhusiwa jana kurudi nyumbani kuuguza majerahaa yake ya miguuni.
No comments:
Post a Comment