KILIMANJARO wakazi wa kata ya Shirimatunda Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamekumbwa na hofu kubwa, baaada ya kufungwa kwa zahanati ya kata hiyo kwa hofu ya kumhudumia mgonjwa anayedaiwa kuwa na virusi vya ugonjwa hatari wa Ebora.
Wakazi hao
wameanza kuhamisha familia zao kwa hofu
ya kukumbwa na ugonjwa, ambao tayari umekwisha
kuua mamia ya watu katika baadhi ya nchi za Kiafrika na Marekani.
Mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amewaondoa hofu wakazi wa mji wa moshi na mkoa wa Kilimanjaro, kutokana
na taharuki iliyoukumba mkoa wa Kilimanjaro hususani mji wa Moshi, ya kuwepo kwa mgonjwa anayehisiwa kuwa na
maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebora.
Gama
alifafanua kuwa mgonjwa huyo ambaye ni mzaliwa wa Marangu wilaya ya Moshi
ambaye makazi yake yako jijini Dar es Salaam, alifika mkoani Kilimanjaro akitokea
Dar es Salaam na alionekana kuwa na homa kali ambapo alitengewa eneo maalumu la
matibabu.
Kwa upande
wake mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa Mwako, amesema kituo cha Shirimatunda
kimewekwa kwa ajili ya tahadhari ya watu wanaohisiwa kuwa na Ebora.
No comments:
Post a Comment