KILIMANJARO wakati serikali
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wakihakikisha wanatokomeza kabisa
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo pamoja na wanawake, mkoani Kilimanjaro matukio ya kubakwa na kulawitiwa kwa watoto
walio chini ya umri wa miaka 10, yamezidi kukuwa kwa kasi.
Matukio hayo
ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakihusiswa na imani za kishirikina, yamezidi
kukua kwa kasi, ambapo yamejidhihirisha baada ya juzi, mtoto mmoja mwenye umri
wa miaka mitatu, kubakwa na mjomba wake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita alisema
kuwa, tukio hilo lililotokea Oktoba 8, mwaka 2014 majira ya saa 10:46 jioni,
katika kijiji cha Sabuko, Kata ya Mbiriri, tarafa ya Siha wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.
Kamanda
Moita alisema kuwa, Mtoto huyo (jina tunalihifadhi), alibakwa na mjomba wake,
aliyetambulika kwa jina la Emmanuel John (16), na kumsababishia maumivu makali
sana sehemu za siri.
“Mjomba wake
huyo, alifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo, ambapo alikuta wazazi wake
hawapo, ndipo alipoamua kufanya tukio hilo la kinyama kwa mtoto huyo na
kumsababishia maumivu makali sehemu za siri,” alisema Moita.
Aidha
Kamanda Moita alisema kuwa, mara baada ya mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho
cha kimyama, alipata maumivu makali
katika sehemu za siri, yaliyomsababishi kukimbizwa katika hospitali ya Kibosho
ambapo amelazwa huko kwa matibabu zaidi.
Pia
Kamanda Moita alisema kuwa, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.
Na Paul Wilium,
No comments:
Post a Comment