KILIMANJARO sakata la kiwanja cha Mawenzi, kilichopo kata ya Mawenzi
manispaa ya Moshi, limechukua sura mpya, baada ya Madiwani wa CHADEMA kuomba
kuitishwa kwa kikao maalumu, kwa lengo la kujadili sakata hilo na kulitafutia
ufumbuzi.
Kikao hicho Maalumu cha Baraza la Madiwani, kililazimika
kugeuka kuwa kamati, kutokana na kuonekana kuwepo kwa tuhuma dhidi ya
mkurugenzi wa Manispaa hiyo Shabaan Ntarambe kuhusiana na uporwaji wa kiwanja hicho.
Akifungua kikao Mstahiki
Meya wa Manispaa hiyo Jafary Michael, alisema lengo la kikao hicho ni kujadili
Hatma ya kiwanja hicho, ili kuwaeleza wananchi ukweli kuhusiana na mmiliki halali wa
eneo hilo.
Alisema ni vema Madiwani wakaweka itikadi za kisiasa
pembeni, kutokana na kwamba wote wamepewa dhamana ya kusimamia na kulinda mali
za wananchi.
Aidha Meya alielezea kusikitishwa kwake, na uwepo wa hisia za vurugu katika kikao hicho, hali
iliyosababisha kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya usalama, wakiwemo askari kanzu, walionekana kurandaranda katika eneo la Manispaa, wakiimarisha ulinzi,
huku wakiwa hawajavaa sare.
No comments:
Post a Comment