DODOMA bunge limeikataa hoja binafsi ya mbunge wa
Kigoma Kusini mheshimiwa DAVID KAFULILA ya kuitaka serikali iwasilishe
bungeni ripoti ya Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kuhusu uchunguzi wa
tuhuma za rushwa katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kwa mujibu wa barua iliyotoka ofisi ya bunge kwenda
kwa mheshimiwa KAFULILA inasema hakuna ibara yoyote ya Katiba wala
kifungu chochote cha sheria kinacholipa bunge madaraka ya kuitaka serikali
iwasilishe bungeni ripoti yoyote ya kiuchunguzi ya TAKUKURU ili ijadiliwe
bungeni.
Aidha suala hilo lilishajadiliwa na kuhitimishwa na
bunge katika mkutano uliopita na bunge lilishatia maazimio yanayotakiwa
kutekelezwa na serikali na TAKUKURU.
Pia katika barua hiyo inasema kuwa kwa mujibu wa
kanuni ya 54 kifungu kidogo cha 4 ya kanuni za bunge inasema hoja yenye lengo
la kutaka kujadili jambo lililokwisha amuliwa na bunge katika kipindi cha miezi
12 iliyopita kabla ya kikao kinachoendelea ifikiriwe tena na haikubaliki labda
kama ni hoja ya kutaka uamuzi huo wa bunge uliokwisha fanyika ubadilishwe.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini
Dodoma mheshimiwa KAFULILA amesema katika bunge lililopita walichojadili na
kufanya maamuzi ni kuhusiana na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali(CAG) kuhusiana na Escrow na sio kuhusiana na taarifa ya TAKUKURU.
No comments:
Post a Comment