Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, March 14, 2015

BAKWATA Kilimanjaro yawakana wamiliki wa vituo vilivyokuwa vimewahifadhi watoto kinyume na sheria

BARAZA kuu la Waslamu (BAKWATA) mkoa wa Kilimanjaro limesema halitambui vituo viwili vilivyogundulika hivi karibuni katika maeneo ya Pasua na Kibosho vikiwa vimehifadhi watoto na kwamba kinachofanyika katika vituo hivyo kina lengo ya kuichafua dini ya Kiislamu.

Kauli ya Bakwata inakuja siku moja baada ya kugundulika kwa kituo kingine katika eneo la Lyamungo wilayani Hai kikiwa na wasichana 11 wenye umri kati ya miaka 14 na 17 na kufanya idadi ya watoto hao kufikia 29 .

Katibu wa Bakwata mkoa wa Kilimanjaro, Rashid Mallya aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa kugundulika kwa nyumba hizo ambazo zinatajwa kama vituo vya kutolea elimu ya Dini ya Kiislamu kwa watoto ni jambo ambalo Bakwata hailitambui.

“Maeneo ya kufundishia dini yetu yanajulikana na si nyumbani kwa mtu,madrasa zetu zinapatikana mahala panapo fahamika ziko misikitini na zinautaratibu wake na kama hazipo msikitini ziko katika maeneo tunayoyatambua ,” alisema Mallya.

Alisema Bakwata kwa sasa inachunguza ili kufahamu ni watu gani wanao endesha vituo hivyo na kwa ufadhili wa watu gani huku akiahidi kutoa maelezo ya kina juu ya kugundulika kwa vituo hivyo siku ya Jumanne.

“Nataka tuonane Jumanne ya wiki ijayo kwa sasa nasafari ya Dar es Salaam ,lakini kifupi madrasa hizo hatuzitambui wala hatujui ni watu gani wanaziendesha,tunataka kuchunguza kufahamu ni watu gani wanao endesha hivyo vituo.” alisema Malya.


Alisema vitu vya namna hiyo vina lengo ya kuchafua dini ya kiislamu na kwamba tayari wamekwisha ichafua huku akisema kuwa kinachofanyika katika vituo hivyo si malengo ya kidini bali ni malengo yao Binafsi.

“Hao watu tayari wamekwisha chafua dini na ni watu ambao hawafahamiki lakini kwa vile hatuwafahamiu kwa sasa hatuwezi zungumza zaidi ,isipokuwa hiki kinachofanyika si malengo ya kidini, hao watu wana malengo yao binafsi ,dini inataratibu zake na inafanya mambo kwa taratibu zinazofahamika.” alisema Malya.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi walisema suala hilo limechukuliwa kiushabiki zaidi hasa kwa pande mbili za kidini huku wakitaadharisha vyombo vya dola kuwa makini katika kufuatilia suala hilo ili lisije sababisha mgogoro usiokuwa na msingi.

Miongoni mwa wananchi ambao wamezungumza na Gazeti hili,Hamis Bakar na Abubakar Salum ambao walisema tatizo linaweza kuwa katika uendeshaji wa kituo bila ya kibali lakini sula la kutoa elimu ya dini kwa watoto hao si tatizo.

“Hiki kitu mie sioni kama kuna tatizo ,kwa sababu kinachofanyika katika vituo hivyo ni jambo jema tu la kutoa elimu ya dini kwa watoto wetu na hili linafanyika kwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo lakini kwa wenye uwezo tunafahamu wengi wao wako nje ya nchi” alisema
Bakar.


Alisema suala hilo liko kidini zaidi na kwamba wapo baadhi ya watu ambao wanatofautiana kiitikadi ndio wamekuwa wakieneza uzushuu juu ya suala hilo ya kuwa watoto hao wamekuwa wakipewa mafundisho ya kuwa Al Kaida wa baadae.

“Tunafahamu zipo madrasa nyingi tu hapa hazina vibali,inazwezekana labda hilo likawa ni kosa la kutokuwa na kibali ,lakini kuna baadhi ya wenzetu hao ndio wanaeneza uwongo juu ya suala hili ya kuwa watoto wanafundishwa masuala ya karate na wengine wanasema kuwa ni Al Kaida.” alisema Bakar maarufu kama jeshi la mtu mmoja.


Naye mmoja wa wazazi ambao watoto hao waliokuwa wamehifadhiwa katika kituo cha Pasua.Abubakar Salum alisema yeye anafahamu motto wake pamoja na mkewe walikuwa wanaenda katika nyumba ile kwa ajili ya mafundisho ya dini na walikuwa wakirudi nyumbani baada ya mafundisho.

“Mimi mtoto wangu pamoja na mke wangu walikuwa wanfundishwa katika kituo hicho na wamekuwa wakienda na kurudi nyumbani kwa ajili ya elimu ya dini ingawaje siwezi fahamu kama wale watoto wengine walikuwa wanasoma masomo ya kawaida pia.” alisema Salum.

Juzi watoto wa kike 11 walikutwa katika kituo kinachojulikana kwa jina la Umm Sukhail kilichopo eneo la Lyamungo,kata ya Kibosho wilayani Hai wakiwa wamehifadhiwa kama ilivyo kuwa kwa watoto 18 waliokutwa katika nyumba moja eneo la Pasua mjini Moshi.

Chanzo: dixonbusagaga Blog.

No comments:

Post a Comment