Hifadhi ya wanyama ya Tarangire ni hifadhi ya wanyama pori
ambayo inapatikana ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, ni hifadhi ya sita kwa
ukubwa kati ya hifadhi zote Tanzania. Hifadhi ya Tarangire ina ukubwa wa hekari
za mraba 2850.
Jina Tarangire limetokana na muunganiko wa maneno mawili kutoka katika kabila la Wamang’ati yaliyounganishwa na kuleta jina hilo ambapo maneno hayo ni Tara na Ngire, neno Tara linamaanisha mto na ngire ni ngiri, ambapo katika hifadhi hiyo kuna mto uliokua na ngiri wengi sana mpaka wenyeji wa eneo hilo kuamua kuuita Tarangire wakimaanisha mto wenye ngiri.
Hifadhi ya Tarangire ipo kilometa 118 kutoka katika jiji la kitalii la Arusha, ambapo hifadhi hiyo ipo upande wa kusini magharibi mwa jiji la Arusha.

Wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya Tarangire ni wengi
sana ila na hifadhi ya Tarangire ndio hifadhi inayoongoza kwa kuwa na idadi
kubwa ya Tembo kuliko hifadhi nyingine zote barani Afrika, pia kuna wanyama
kama Simba, Chui, Nyumbu, Tumbili, Nyati, Twiga, Punda milia, na wengine wengi.
Unaweza kutembelea hifadhi ya Tarangine kwa siku moja, mbili au tatu kulingana na unachopenda kukiona katika hifadhi hiyo, kwasababu ni vigumu kuweza kwa wageni au wenyeji kuweza kutembea kilometa za mraba 2850 kwa siku moja mpaka tatu. Wageni wengi wanaoingia katika hifadhi ya serengeti hutembelea sehemu ndogo sana ya hifadhi hiyo.

Utaratibu au sheria za kuingia na kutembelea hifadhi ya
Tarangire zimeandikwa kwenye bango kubwa lililopo katika geti la kuingilia
kwenye hifadhi hii. Kwa muongoza watalii au mgeni yeyote anashauriwa kusoma
utaratibu au sheria hizo kabla ya kuingia katika hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment