Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, March 7, 2015

Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) yasisitizia umuhimu wa watanzania kufanya utalii wa ndani

KILIMANJARO hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), imekiri kuwepo kwa idadi ndogo ya watanzania wanaofika na kuupanda mlima huo jambo ambalo limekuwa likichangia kutokuwepo na mwamko mkubwa wa utalii wa ndani.

Hayo yalisemwa na mkuu wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Erastus Lufungulo, wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa Maafisa wa Jeshi la magereza ambao wamepanda mlima huo kwa ajili ya kuwahamasisha watumishi wa umma na sekta binafsi kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Lufungulo alisema kuwa bado kuna mwamko mdogo wa watanzania katika utalii wa ndani, na kwamba kati ya watalii elfu hamsini wanaofika katika kuupanda mlima Kilimanjaro, asilimia tano tu ni watalii wa ndani ya Tanzania wanopanda mlima huo.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi bendera kwa maafisa 19 wa jeshi la magereza, Kamishna wa Jeshi la Magereza hapa nchini, Jenerali John Casmir Minja, ametoa rai kwa watanzania kuona umuhimu wa kutembelea vivutio hivyo hali ambayo itaongeza hamasa kubwa katika utalii wa ndani.

Alisema upandaji wa mlima huo ni zoezi endelevu ambapo kila mwaka wamejiwekea malengo ya kuupanda mlima ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani, ikiwa ni pamoja na kuwaweka kuwa tayari wakati wa kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga afya na kuilinda miili na maradhi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa magereza hapa nchini, Kamishna msaidizi mwandamizi SACP Venant Kayombo, amesema ni vyema serikali ikaweka utaratibu maalumu wa kuwaruhusu watumishi wa umma kupata fursa ya kuupanda mlima ili waweze kuutangaza utalii wa ndani.

Kamishna msaidizi wa Gereza la Karanga Dkt Hassan Mkwiche na Mkaguzi wa Gereza Deodatus Kazinja, ambao wamepanda mlima huo walisema kuwa wamejiandaa kikamilifu katika kuutangaza utalii wa ndani na kwamba watakuwa mabalozi wazuri katika kuwahamasisha watumishi wengine kuona umuhimu wa kuupanda mlima huo.

No comments:

Post a Comment