Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, March 10, 2015

Marie Stops Tanzania wakemea imani potofu na taarifa zisiso sahihi juu ya uzazi wa mpango

KILIMANJARO imani  potofu na taarifa zisizo sahihi miongoni mwa kina mama juu ya uzazi wa  mpango  umefanya kina mama wengi kuwa waoga  wakutumia uzazi wa mpango.
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Moshi  Novatus Mkunga alipokuwa ana mwakilisha mkuu wa mkoa wa kilimanjaro katika  uzinduzi wa Huduma ya Mkoba wa uzazi wa mpango ulioratibiwa na "Marie Stops Tanzania", ulifanyika katika wiliya ya Hai alisema kuwa woga huo unasababisha ongezeko kubwa la watu nchini.
Kasi ya ongezeko la watu ni kubwa kwa sasa nchini kuliko ongezeko la uchumi. Uzinduzi wa huduma ya mkoba wa uzazi wa mpango utasidia kudhibiti ongezeko hilo kwa vile mkoba huo utakuwa unatembea kila mtaa na kutoa elimu sahihi juu ya uzazi wa mpango hivyo itasaidia kasi ya uchumi wetu .
Alisema huduma hiyo itasaidia wazazi kupata watoto wanaoweza kuwamudu kwa kuwapa elimu na malazi kama inavyopaswa na kuondokana na  taifa la  watu  tegemezi na dhaifu katika shughuli za kimaendeleo  hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknologia.
Utafiti unaonesha kwamba matumizi sahihi ya uzazi wa mpango unapunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi kwa  asilimia 35  mpango unaotakiwa ni kupunguza vifo vya kinamama na dada zetu ambao ni rasimali kubwa katika jamii yetu.

Huduma hii ikiwa karibu sana na wananchi huduma za wananchi zitaboreka  na  kuongeza maendeleo kwa mkoa wetu wa kilimanjaro na taifa kwa ujumla ni vyema wananchi wakatumia  fursa hii kwa manufaa yao.
Amewataka wanaume kuwa bega kwa bega  na wanza wao kutumia uzazi wa mapango na kuwataka  viongozi wote wa mkoa hasa wa vijiji na mitaa kutoa  ushirikiano wakutosha  kwa "Marie Stops Tanzania" wanapokuwa kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka "Marie Stops Tanzania" Bi. Anna Shana alisema takwimu  zinaonesha takibrani wanawake elfu nane wanakufa kila mwaka  kutokana na matatizo ya uzazi jambo ambalo halikubaliki katika jamii yetu.
Kwa kutumia  uzazi wa mapango unaweza kuzuia mimba zisizotarajiwa na hivyo huzuia vifo hivyo kwa kiasi kikubwa na pia kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Uzazi wa mapango una maana katika maendeleo na una mchango mkubwa katika maisha sio kwa wazazi tu, bali na  vijana ambao ni taifa la leo na kesho asilimia 16 ya  vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 wametumia uzazi wa mapango, na asilimia 25 ya vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 wanapata mimba  kila mwaka.
"Marie Stops Tanzania"  tunaamini kuwa vijana wanaweza kufikia malengo yao kama wakitumia uzazi wa mpango kwa kufuata ushauri utakaotolewa na wataalamu  wa afya.

Amewataka wazazi, waalimu pamoja na walezi kuwashauri vijana juu ya uzazi wa mpango pia  kusaidia serikali  kufikia malengo ya milenia  
"Marie Stops Tanzania" watakuwa wanatoa elimu na huduma ya uzazi wa mapango bure kwa jamii.

Na Queen Isack,
Kilimanjaro Official Blog.

No comments:

Post a Comment