KILIMANJARO ikiwa bado
wananchi mkoani Kilimanjaro wakiwa na hali ya sintofahamu, kuhusiana na tukio la kuhifadhi watoto 18,
ndani ya nyumba moja kinyume na sheria za nchi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limegundua tena
nyumba nyingine huko wilayani Hai iliyokuwa ikiwahifadhi watoto 11 na
kuwafundisha masomo ya dini ya kiislam na Ushonaji.
Jeshi hilo limegundua nyumba hiyo iliyopo
katika kijiji cha Lyamungo wilayani Hai,
siku ya jumatano baada ya jeshi hilo kupokea taarifa kutoka kwa
wasamaria wema ambapo jeshi la polisi lilifika katika nyumba hiyo na kukuta watoto 11, wa
kike wenye umri kuanzia miaka 14 hadi 17.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, Kamanda Mwandamizi wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geoffrey Kamwela,
alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa hizo, walifaka katika nyumba hiyo
inayomilikiwa na Abubakari Juma(64), Mwalimu mstaafu wa shule za Msingi
ambaye alifungua shule hiyo na kuipa jina la UMM SUKHAIL.
Kamwela alisema kuwa, watoto hao
walikuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya Kiislam pamoja na Ushonaji ambapo
walikuwa wakilala katika nyumba hiyo.
“Kweli tumegundua nyumba nyingine
ambayo inafanya kazi ya kuwahifadhi watoto na kuwafundisha masomo ya dini
pamoja na Ufundi cherehani kinyume na sheria ambapo mwenyenyumba na watoto
hao wapo katika kituo cha polisi Moshi kati” alisema Kamwela.
Aliongeza kuwa katika uchunguzi wa
awali na mahojiano ya watoto hao, inaonesha kuwa wanatoka katika mikoa ya
Dodoma, Singida, Tanga, Tabora, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.
“Kama mtakuwa na kumbukumbu nzuri,
katika tukio la kwanza la watoto 18, ukiangali mikoa waliyotoka na hili pia
utagundua kuwa wote wametoka mikoa hiyo hiyo sasa nashindwa kuelewa kuwa hawa
wamiliki wa nyumba hizi mbili wanafanya kazi pamoja au” alisema Kamwela.
Kamanda huyo aliwataja watoto hao
kuwa ni Amina Yahaya(16),Mariam Issa(14), Zainabu Rajabu(16), wote wakazi wa
Arusha, Idia Rashidi(15), mkazi wa Mbeya, Amina Adam(14), mkazi wa Tanga,
Rehema Idd(16), mkazi wa Singida,Nasra Bashiri(16), mkazi wa Kilimanjaro.
Wengine ni Shahila Abdi(14), Salma
Athumani(16), wote wakazi wa Dodoma, Hadija Ally(17), mkazi wa Mtwara, Amina
Muhamedi(18).
Aliendelea kueleza kuwa, mmiliki
wa nyumba hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro, kwa uchunguzi zaidi ili kubaini
kuwa shule hiyo aliyokuwa akiwafundishia watoto hao ipo kisheria na
imesajiliwa pamoja na kutambua utoaji wa vyeti vya wanafunzi hao pindi
wanapoitimu mafunzo.
Alisema kuwa endapo kutaonekana
kuwa, mmiliki wa nyumba hiyo atakuwa amevunja sheria yoyote basi atafikishwa mahakamani na sheria kufuata mkondo wake.
No comments:
Post a Comment