KILIMANJARO serikali imeahidi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
yanayojitokeza mara kwa mara ili kuepusha majanga yanayojitokeza hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa
wilaya ya Siha, Dkt Charles Mlingwa, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa
Matokeo ya utekelezaji wa Mradi wa kupunguza uharibifu wa Ardhi katika sehemu
za miinuko ya mlima Kilimanjaro, mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uhuru hotel mjini Moshi.
Alisema mradi wa matumizi
endelevu ya ardhi (SLM), umeweza kuwa na mafanikio makubwa kutokana na juhudi
kubwa ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kwa kushirikisha sekta binafsi na
mashirika yasiokuwa ya kiserikali.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa
matumizi endelevu ya ardhi mkoa wa Kilimanjaro, Damas Masologo alisema kuwa
utekelezaji wa miradi hiyo kwa mkoa umefanikiwa kwa asilimia 70.
Awali akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa mradi, Msimamizi wa mradi kutoka (UNDP), Getrud Lyatuu alisema
miradi hiyo ilikuwa ni miradi ya majaribio, katika sekta ya Kilimo, utunzaji wa
mazingira uzalishaji mali, na ufugaji.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Siha,
Rashid Kitambulilo, alisema miradi ya SLM, imekuwa na mafanikio makubwa, na
kwamba halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 150 ili kuendeleza
utekelezaji wa miradi katika ambyao hayafikiwa na mradi.
Mkutano huo wa kanda umezishirikisha
nchi za Uganda , Malawi, Kenya na wenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment