Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, March 8, 2015

Wadau wa Elimu mkoani Kilimanjaro waendelea kutoa misaada kwa watoto wanaoishi katika azingira magumu

KILIMANJARO wadau mbalimbali wa elimu mkoani Kilimanjaro wameendelea kusaidia sekta ya Elimu, ambapo kada wa CCM Olivya Sanare, amechagia vifaa mbalimbali vyenye thamini ya milioni 1.6, kwa shule ya msingi Kimanganuni iliyopo kata ya Uru wiulayani Moshi.

Kada huyo aliamua kutoa msaada huo, baada ya kuona wapo watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wanashindwa kuendelea na masomo kutoka na sababu mbalimbali.

Misaada aliyokabidhi kada huyo ni pamoja na madaftari 1800, chaki boksi 10, kalamu zaidi ya 700, Makaratasi ya kufanyia mitihani "Rim papers" 10, madaftari makubwa "Counter book" 200, pamoja na vifaa nya kujisitiri kwa ajili ya watoto wa kike katoni 10.

Mara baada ya kukabidhi misaada hiyo, Sanare alisema kuwa, ameamua kutoa misaada hiyo kwa watoto hao yatima na wasiojiweza ili waweze kujiona kuwa nao wanathaminika na kujiona sawa na watoto wengine.

Alisema wapo watoto ambao wanania ya kusoma, lakini kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha au kuwa yatima wamekuwa wakishindwa kuendelea na masomo.

“Watoto wa mitaani sio wamependa wao wenyewe, wengine walikuwa wanatamani sana kusoma ila wamekosa wa kuwasomesha ndio maana unasikia kuna vikundi vinaibuka wanajiita Panya Road, ila jamii inapaswa kuamaka na kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu” alisema Sanare.

Kada huyo aliahidi kuhakikisha atawasaidia watoto watatu wanaosoma katika shule hiyo, ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, hadi watakapofanikiwa, na kuahidi kama watashinda kufaulu darasa la saba atawasomesha fani itakayowasaidia maishani mwao.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Halima Lyimo, aliwataka wadau wengine wa elimu na taasisi mbalimbali kuiga mfano huo, ili kuwawezesha watoto wanaioshi katika mazingira magumu na yatima kupata elimu.

“Kweli huku kwetu kunawatoto wengi wamekuwa wakiacha shule kutokana na kukosa wa kuwasomesha, unakuta mwanafunzi kafaulu kwenda sekondari lakini mzazi wake hana kipato cha kumpeleka Sekondari hivyo anakaa nyumbani tu anakuwa ni wakukatia ng’ombe majani” alisema Halima.

No comments:

Post a Comment