Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 9, 2015

WADAU WA MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA WATOA MISAADA KWA WAZEE WASIOJIWEZA

Mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo Media  Krantz Mwantepele akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kufika katika kituo cha wazee wasiojiweza Msimbazi  kinachosimamiwa na jimbo kuu hapa dar es salaam kanisa la katoliki na kuhudumia wazee wapatao kumi na moja waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu.Timu nzima ya Mwanaharakati Mzalendo Media ilikuja hapa kuwaona wazee hawa na kupata nafasi ya kuwafariji na kutoa baadhi ya misaada ya chakula na nguo za kuwasitiri leo siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.
Mdau Marko Mlonganile akipata nafasi ya kumsalimia mmoja ya wazee wanaopatikana katika kituo hiki na kupata nafasi ya kujua baadhi ya changamoto zinazopatikana katika kituo hiki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015
Mdau subilaga james akiwa  katika taswira na mmoja bibi wanaopatikana katika kituo hiki cha wazee wasiojiweza kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam la kanisa katoliki na kuweza kuhudumia wazee wapatao  kumi na moja  siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.

Bibi ambaye ni mmoja ya wazee wanaotunzwa katika kituo hiki akitabasamu baada ya wadau wa Mwanaharakati Mzalendo Media kutembelea  hapa na kuweza kuwafariji kwa kukaa nao na pia kutoa mahitaji kwa ajili ya chakula na nguo za kuwasitiri katika kituo cha wazee wasiojiweza hapa jijin dar es salaam kituo kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam katoliki   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015

Bibi akitabasamu baada ya wadau wa Mwanaharakati Mzalendo Media kutembelea  hapa na kuweza kuwafariji kwa kukaa nao na pia kutoa mahitaji kidogo kwa ajili ya chakula na nguo za kuwasitiri katika kituo cha wazee wasiojiweza hapa jijin dar es salaam kituo kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam katoliki   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.

Baadhi ya wadau toka Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakiongea na mmoja ya wazee aliyelala kitandani ni moja kati ya wanaotunzwa na kituo cha wazee   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.

Moja ya nyumba ambayo inatunza wazee wasiojiweza na ni kituo kinachosimamiwa na kanisa katoliki jimbo kuu dar es salaam.

Mahojiano yakiendelea na msimamizi wa kituo hiki sister angelina hapa akieeleza historia fupi ya kituo na jinsi wanavyowahudumia wazee katika kituo hiki.
Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media Krantz Mwantepele akitoa maelezo kidogo kwa msimamizi wa kituo hiki sister angelina  (hayupo pichani ) na wanaosikiliza kwa makini ni wadau Subilaga na Happy 

Wadau wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakifurahi jambo na msimamizi wa kituo hiki sister angelina.

Tukikabidhi baadhi ya michango kama mahitaji muhimu ya chakula kwa mismamizi wa kituo cha wazee wasjiojiweza sister angelina  anayeshuhudia ni mdau bensoni.
Mmoja wa wazee akiongea jambo mdau Marko mlonganile  huku  mkurungezi mtendaji  wa Mwanaharakati Mzalendo media Krantz Mwantepele akisikiliza kwa makini.
Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media krantz mwantepele  akikabidhi baadhi ya misaada ya chakula na nguo  kwa msimamizi wa kituo hiki siter angelina  iliyotolewa na wadau wa mtandao wa Mwanaharakati mzalendo Blog.

Mkurungezi  wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA Krantz Mwantepele  akiwa katika picha ya pamoja na wadau   walioshiriki baada ya kumaliza safari ya kuwaona wazee katika kituo hiki na kutoa baadhi ya mahitaji ya chakula na nguo za kuwasitiri


PICHA ZOTE  NA ALFRED MLONGANILE 

No comments:

Post a Comment