Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, March 29, 2015

Wananchi wafunga offisi ya Serikali ya kijiji kwa kumtuhumu Mwenyekiti wao kutoshirikiana nao

KILIMANJARO baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Ormelili Kata ya Orkolili Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro wamefunga ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho kwa madai mbalimbali wanayo mlalamikia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Jeremiah Laizer  ikiwamo kutaka kuweka mnara wa simu wa kampuni ya Vettel Compony bila kuwashirikisha.

Wakiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya kijiji hicho  na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali  ktuka katika jamii za wafugaji.

Mwananch hao, walisema kwamba hawapo tayari kufungua ofisi hiyo hadi hapo mwenyekiti huyo atakapo washirikisha katika ujenzi huo wa mnara.

Mmoja wa Wananchi hao alisema kuwa "hatuna imani na uongozi huu kwa kuwa wanafanya  maamuzi binafsi bila kutushirikisha na tuna tetesi za kutosha  kuwa mnara huo wa simu sio salama kwa afya zetu na ndiyo maana wamefanya kimya kimya pia wamepokea fehda katika mradi huo."

Akizungumzia kuhusu sakata hilo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho ambaye amekaimu Joakimu Panga alisema kuwa serikali ya Kijiji ilikubali pendekezo hilo la ujenzi wa mnara  lipelekwe kwa wananchi, lakini cha kushangaza wananchi hawakupewa taarifa hiyo ya ujenzi wa mnara.

Akijibu malalamiko hayo mweneyekiti wa kijiji hicho Jeremiah Laizer pamoja na mjumbe wa kamati ya fedha Noel Mollel, walisema kuwa wamefuata utaratibu zote kutoka ngazi ya halmashauri kwa mkurugenzi Rashidi Kitambulio, inayowaruhusu kujenga mnara katika eneo hilo na

Pia wananchi tumewashirikisha tunashanga wanafunga ofisi, hizi ni chuki za baadhi ya watu walioshindwa katika uchaguzi uliopita lengo ni kutukwamisha.

No comments:

Post a Comment