KILIMANJARO katika tukio la kustaajabisha lililotokea tarehe 7 Machi mwaka huu, huko maeneo ya Pasua mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo watoto 18 walikutwa wakiwa wamehifadhiwa katika nyumba
moja kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda Mwandamizi wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geoffrey Kamwela, alisema kuwa "Machi 07 mwaka huu, majira ya saa 7:30 za mchana, jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mmiliki wa nyumba moja aitwae Aisha Wilium akiwa anahifadhi watoto kinyume na sheria."
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda Mwandamizi wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geoffrey Kamwela, alisema kuwa "Machi 07 mwaka huu, majira ya saa 7:30 za mchana, jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mmiliki wa nyumba moja aitwae Aisha Wilium akiwa anahifadhi watoto kinyume na sheria."
Mmiliki huyo alikuwa anawahifadhi
watoto hao wenye umri kuanzia miaka 2-14, kinyume na sheria na kuwafundisha
mafunzo ya dini ya kiislam aliongeza RPC.
Kamwela aliwataja watoto hao kuwa
ni Sumaiya Ayubu(12), Osama Ayubu(10), Mwanafunzi wa darasa la Kwanza, Yasri
Abedi(8), mwanafunzi wa darasa la pili, wote wanasoma shule ya msingi
Jitegemee iliyopo kata ya Pasua.
Wengine ni Udhaifu Ramadhani(10),
darasa la tatu, Athma Ramadhani(8), darasa la pili, wote wanasoma Azimio
iliyoko Pasua, Warda Gabriel(11), mwanafunzi wa shule ya Msingi Kaloleni
ambaye paka sasa wazazi wake hawajulikani.
Amina Ally(14), amemaliza darasa
la saba katika shule ya msingi Langasani, Shaima Shabani(11), mwanafunzi wa
darasa la 5 katika shule ya msingi Pasua, Saumu Mustafa(14), amemaliza darasa
la saba shule ya msingi Pasua, Zawiya Shabani(14), amemaliza darasa la saba
Jitegemee, Zahara Ramadhani(13), amemaliza darasa la saba Azimio.
Aliendelea kuwa, Yasini
Abdalla(7), mkazi wa Pasua-Matindigani, Fariha Mustafa(6), mkazi wa Mwanza,
Marsadi Mstafa(3), Farihia Mustafa(2), Musa Mustafa(5), Abuu Mustafa(3), wote
wakazi wa Pasua, na Halima Abdi(20), mkazi wa Tanga ambaye ndiye alikuwa
akitumika kama mtoa huduma.
Katika uchunguzi wa awali
imebainika kuwa watoto hao walikuwa wakiishi katika mazingira magumu,
kutokana na kulala watoto wane katika kitanda kimoja, huku wengine
wakitandikiwa magodoro sakafuni.
Kamanda Kamwela alisema kuwa,
watoto wote wametambuliwa na wazazi wao na kukabidhiwa isipokuwa mtoto mmoja
ambaye mpaka sasa wazazi wake hawatambuliki.
Upelelezi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea, huku mmiliki wa nyumba hiyo anashikiliwa na Jeshi hilo alisema Kamanda
Kamwela.
No comments:
Post a Comment