John Mnyika, mbunge wa jimbo la Ubungo. (Picha kwa niaba ya maktaba)
DODOMA spika wa Bunge ameahirisha kikao cha bunge kwa muda usio julikana baada ya kutokea kwa vurugu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa upinzani.
Vurugu hizo zilitokea baada ya mbunge wa Ubungo mheshimiwa Jhn Mnyika, kusimama na kuomba kutoa hoja binafsi ya kusitisha shughuli za bunge zilizopangwa ili kujadili jambo la dharura.
Mheshimiwa Mnyika ameomba kutoa hoja kwa kutumia kifungu cha 47 kifungu kidogo cha kwanza akiiomba serikali kutoa majibu kuhusiana na zoezi la uandikishwaji katika daftari la wapiga kura kwa kutumia mashine ya kielektroniki(BVR) ambalo bado halijakamilika katika mkoa wowote mpaka sasa.
Akijibu hoja hiyo spika Makinda amemtaka mheshimiwa MNYIKA kukaa chini ili shughuli ziendelee na baadae ufafanuzi utatolewa hali iliyoanzisha vurugu na kulazimika kuahirisha shughuli za bunge.
Awali mbunge wa Kisarawe mheshimiwa Suleman Jaffo, ameiomba serikali kuhakikisha inaleta hati ya dharura katika Mkutano wa 20 wa bunge ambapo amependekeza Serikali ipeleke muswada wa hati ya dharura wa kupitisha katiba ya mpito itakayokuwa na mambo manne yanayohitajika katika uchaguzi mkuu ujao .
Ametaja mambo hayo kuwa ni kuwe na tume huru ya uchaguzi,matokeo ya rais kupingwa mahakamani, eneo la kupata mgombea binafsi na umri wa bunge.
Akijibu hoja hiyo spika Makinda, amesema itajibiwa baadae wakati waziri mkuu atakapokuwa anaahirisha bunge.
No comments:
Post a Comment