KILIMANJARO vijana wa wilaya Siha, mkoani kilimanjaro, wametakiwa kutafuta mbinu mbalimbali za maendeleo zitakazo wawezesha kujishuhulisha na kujiingizi kipato na kuachana na unywaji wa pombe kupindukia.
Imaelezwa
kuwa vijana wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwa ajili ya kunywa
pombe badala ya kufanya kazi na kwamba hali hiyo inasababisha
wajihusishe na vitendo vinavyo hatarisha maisha yao.
Mwenyekiti wa
Kijiji cha Sanya Hoyeee, wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro, Moses Munuo
alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, kuhusu changamoto zinazokwamisha maendeleo ya vijana katika
wilaya hiyo.
Aliwataka vijana kujenga utamaduni wa kufanya kazi na
kusoma, badala ya kutumia muda mwingi kunywa pombe na kucheza pool table. Ambapo baada ya kulewa wanajiusisha na vitendo viovu ikiwamo ngono
na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa kama ukiwepo UKIMWI.
Hivyo
kuwaomba vijana kubadilika na kutumia muda mwingi kufanya matendo mema
yanayompendeza mwenyezi Mungu ili waishi kwa amani katika dunia hii.
Pia
aliwataka wananchi wilayani humo kupanda miti kwa wingi hasa maeneo
yanayowazunguka, alisema asilimia 17 hadi 20 ya mabadiliko ya tabia nchi
yanasababishwa na ukataji miti na uharibifu wa mazingira unaoendelea
katika nchi zinazoendelea.
Amewaomba wananchi wilayani humo
kupanda miti kwa wingi pamoja na ya matunda kuzunguka katika maeneo ya
wazi hasa katika kipindi hichi cha mvua.
No comments:
Post a Comment