KILIMANJARO wazee wa kijiji cha Losaa, kata ya Masama Magharibi, wilayani Hai, mkoni Kilimanjaro wametoa malalamiko yao kwa uongozi wa wazee wilaya kuhusu kunyimwa kitafunwa(kiporo) asubuhi na wake zao.
Wametoa
malalamiko hayo leo katika kikao cha wazee wenye umri wa miaka 60 na
kuendelea kilicho lenga kuibua changamoto wanazo kutana nazo kwa maisha
ya sasa ikiwa ni pamoja na kujadili lishe bora na matibabu kwa Wazee.
Wamesema kuwa zipo changamoto nyingi zinazo wakumba likiwemo la kutokupata kifungua kinywa asubuhi wanacho kiita kiporo, pamoja na chakula chenye virutubisho vizuri kwa wazee ikizingatiwa kuwa wanahitajika kutunzwa na jamii iliyo wazunguka.
“Jamani
asanteni kwa kufika leo kijijini kwetu nazungumza kwa masikitiko kuwa
huku vijijini tunapata taabu kubwa ya chakula kwani baadhi ya wanawake
hawatupi kiporo asubuhi licha ya chakula kuwepo nyumbani jambo ambalo
lina tulemaza sisi wazee na Serikali yetu ipo tufanyeje?” alisema na kuhoji mmoja wa wazee hao wa kiume katika kikao hicho.
Waliongeza
kuwa wazee kutokupata chakula katika jamii kunawasababishia kuishiwa na nguvu kwa
haraka hivyo wazee kuonekana kuwa siyo hazina katika jamii ya leo
kutokana na wao kuchoka mapema hivyo kuitaka Serikali kuhakikisha kuwa
wazee wanathaminika kwa kupewa chakula bora na matibabu ili wazidi
kuwepo na kuwa hazina.
Kwa upande wake katibu wa Wazee Wilaya
Shikenaufoo Lema aliwataka wazee hao kutoa taarifa kwa uongozi wa
kijiji juu ya masuala ya kunyimwa chakula na wake zao ili waweze
kusaidika kwa haraka huku wazee kwa upande wa wanawake wakihitajika
kuonesha upendo kwa familia zao hasa ikionekana wote ni wazee ili
kuepuka aibu.
“Naiomba jamii ya watanzania ambao siyo wazee kwa
sasa watambue kuwa uzee upo na utakuja kuwakuta hivyo kuwataka waweze
kuwa na mapenzi mema kwa jamii ya wazee ili wazee waweze kuwa hazina kwa
sasa na baadae.” Alisema Lema.
No comments:
Post a Comment