Mbunge wa jimbo la Hai Mheshimiwa Freeman Mbowe
KILIMANJARO wito umetolewa kwa Wananchi Mkoani Kilimanjaro kujenga utamaduni wa kusaidia Watu wasiojiweza kwenye Jamii wakiwamo Watoto yatima ,Walemevu, Wazee na Wajane.
KILIMANJARO wito umetolewa kwa Wananchi Mkoani Kilimanjaro kujenga utamaduni wa kusaidia Watu wasiojiweza kwenye Jamii wakiwamo Watoto yatima ,Walemevu, Wazee na Wajane.
Haya yalisemwa jana na Zakaria Mushi Katibu wa Kikundi cha Express Vikoba cha Kijiji cha Lukani, Kata ya Masama Magharibi, Wilayani Hai, Mkoani Kilimanjaro wakati wa kikao cha kawaida cha kikundi hicho kilichofanyika katika ofisi ya kijiji hicho.
Mushi alisema katika Jamii za Watu kumekuwa na makundi ambayo yanaitaji msaada mkubwa kutoka kwa wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamejaaliwa kuwa kipato na afya.
Alisema kuwa ni wajibu wa watu hao wa aina hiyo kuwasaidia wale wanaoitaji kama vile watoto yatima, Walemavu, Wazee na Wajane.
Mmoja wa Wazee wa kikundi hicho alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo kutelekezewa familia na Vijana wao, vijana wanaoa kisha wanatelekeza familia na kwenda mikoa mingine kutafuta maisha wakatisisi wenyewe ni wakutunzwa vijana wengi wa mkoa wa kilimanjaro wanatabia hiyo ya kuacha familia hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo.
Pia wamemtaka Mbunge wa Jimbo hilo Freeman Mbowe kufika katika Kijiji hicho na kwenda kuwatembelea wazee hao kwani toka wamchague hajawaifika katika eneo hilo.
Kawa upande wake Mwenyikiti wa Kikundi hicho Mashoya Natai aliiomba Serikali kuhakikisha inasimamia utoaji wa huduma kwa wazee katika vituo mbalimbali vya Afya ,alisema vituo vingi vya afya vinachangamoto nyingi kwa wazee
Natai alisema kuwa ni bora serikali ikazinngatia kusimamia huduma za afya kwa wazee ili huduma hiyo iweze kutekelezwa kwani bado kuna sehemu nyingi huduma hizo zimekuwa ni kitendawili
Bado huduma ya matibabu kwa wazee baadhi ya maeneo ni changamoto licha ya serikali kusema wazee watibiwe bure alisema Natai
Pia alisema kuwa masuala ya wazee yaingizwe kwenye bajeti za halmashauri ili kuweza kupunguza makali dhidi ya wazee hao
Aliongeza kwa kuyaomba mashirika na Taasisi mbalimbali, kuchangia katika ujenzi wa jengo la Wazee,yawatoto yatima na wale wanaoishi katika, ili kuweza kulifanikisha na kulimaliza kwa jengo hilo
No comments:
Post a Comment