KILIMANJARO mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imemhukumu mkazi wa kijiji cha Sanya Juu, Wilaya ya Siha, Christopher Raphael (30) kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 9
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Denis Mpelembwa, mbele ya mwendesha mashtaka wa polisi Roymax Membe, alisema kuwa anatoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushaidi uliotolewa mahakamani hapo usioacha shaka yoyote wa mashaidi watano wa upande wa mashtaka akiwemo Daktari wa hospitali ya Kibong’oto wakiongozwa na mwendesha mashtaka wa polisi Membe.
Ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa polisi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Februari 2 mwaka 2013 majira saa 9 alasiri katika Meneo ya Kitongoji Cha Mabanzi ambapo alimlawiti mtoto huyo chini ya miaka 12 akiwa na akili alimfanyia tendo la ngono kinyume na maumbile mtoto wa miaka 9.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mwendesha mashtaka Membe aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa kutokana na kitendo alichokifanyiwa mtoto huyo kimemuathiri kisakilojia na kuathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wake katika maisha.
Alisema matendo ya ukatili dhidi ya watoto ikiwamo vitendo vya ngono vinaonekana kuwa janga la kitaifa hivi licha ya jitihada za serikali, taasisi binafsi na wanaharakati kuunganisha nguvu zao bado matendo hayo yanazidi kuongezeka.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na umri wake pamoja na kuwa na watoto wanaomtegemea ombi ambalo mahakama hiyo ililitupilia mbali.
No comments:
Post a Comment