Kampuni ya Uuzaji wa Mafuta ya Panone And co. Ltd inayofanya biashara ya mafuta ya magari na bidhaa mbalimbali leo imeshiriki katika Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Meimosi zilizoadhimishwa Kimkoa ndani ya Viwanja vya chuo cha ushirika. Katika Sherehe hizo makampuni mbalimbali na taasisi yalipata fursa ya kuelezea Bidhaa zinazozalisha.
Maandamano ya Magari ya Kampuni ya Panone yakipita katikati ya mji wa Moshi.
Kwa mwaka huu kampuni ya Panone ilishiriki Maadhimisho hayo huku ikiwa na lengo la kutambulisha Bakery yao ya kisasa inayotengeneza Mikate, Maandazi, Donati, Crips, Popcon, Cake nk. Akitoa maelezo juu ya Bakery hiyo Ofisa habari wa Panone ndugu Cassim Mwinyi aliweza kuelezea ubora wa Bidhaa zinazozalishwa na Kampuni hiyo huku akiwasisitiza wafanyakazi na wananchi kutembelea supermarket za Panone zilizopo katika kila kituo cha mafuta cha kampuni hiyo na kununua bidhaa hizo ili kuthibitisha ubora wake.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Panone wakiwa katika Maandamano.
Baada ya kufanya uwasilishaji Kampui hiyo iliweza kutoa zawadi ya bidhaa zao kwa wafanyakazi walioshiriki Maadhimisho hayo. Mwisho wa Maadhimisho hayo Tuzo hutolewa kwa kampuni iliyofanya uwasilishaji vizuri na ubora wa bidhaa husika. Katika Tuzo za Uzalishaji Kampuni ya Panone ilipata nafasi ya tatu kati ya kampuni na Taasisi zaidi ya hamsini zilizoshiriki tukio hilo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Panone wakifurahia baada ya kutangazwa washindi wa uzalishaji wa bidhaa bora.
Mfanyakazi wa Panone ndugu Mdoe akipokea zawadi ya Kikombe toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mh. Novatus Makunga.
Wafanyakazi wa Panone wakiwa katika picha ya pampaada ya kukabidhiwa kombe
Meneja wa kampuni ya Panone ndugu Gido Marandu akionesha tuzo ya kombe walilokabidhiwa.
Akizungumza na Mtandao huu baada ya Ushindi huo Meneja wa Kampuni ya Panone ndugu Gido Marandu alisema Kampuni ya Panone imejipanga kutoa huduma bora na kuwaletea bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kimataifa huku akisisitiza wateja kutumia bidhaa zao na kupaa hduma zao.
Wananchi wakifurahia zawadi za bidhaa za Panone Bakery walizopewa na Kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment