Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi mkoani Mara wakijiaanda kuanza maandamano kutoka Hospitali Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Musoma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi wilayani Musoma wakiwa wamekusanyika nje ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma kwenye viwanja vya Mkendo, mkoani Mara.
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga kutoka mikoa mbalimbali ya nchini wakijumuika na wenyeji wao kwenye maandamano ya maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wakunga wakijumuika na wakinama wa mjini Musoma njiani kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo wakati maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani burudani ya matarumbeta yaliyokuwa yakishereheshe maandamano hayo.
Wakunga wa kiume kutoka wilaya ya Serengeti wakiwa wamejumuika na wenyeji wao kwenye maandamano hayo.
Shangwe zikiendelea kuelekea viwanja vya Mkendo.
Kinababa nao hawakubaki nyuma waliwaunga mkono Wakunga kwenye maandamano hayo.
Mkazi wa mjini Musoma mwenye ulemavu aliyejumuika kwenye maandamano hayo akisukumwa na mmoja wa Wakunga kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo zinakofanyika sherehe za maadhimisho hayo.
Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige naye alishiriki maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma mkoani Mara.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) Tanzania, Sawiche Wamunza (wa kwanza kulia) akishiriki kwenye maandamano hayo.
Mpiga picha wa Clouds TV Ntibashima Edward akiwa amepanda juu ya gari aina ya canter kwa ajili ya kuchukia matukio ya maandanamano hayo.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) wakipokea maandamano kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mjini Musoma, Mkoani Mara. Kutoka kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali, Dk. Ama Kasangala, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magese Mulongo, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Musoma, Stephen Zelote pamoja na Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Bi. Feddy Mwanga.
Maandamano kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yakiwasili kwenye viwanja vya Mkendo na kupokea na mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) yakitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma.
Picha zote na Zainul Mzige
No comments:
Post a Comment