Ndugu watanzania wenzetu, tunapenda kuwapongeza
kwa kumaliza mchakato wa kampeni za vyama vya siasa na wagombea kwa
amani na utulivu. Vile vile tunawapongeza kwa kupiga kura kwa kwa amani
na utulivu, kwani pamoja na kujitokeza kwa wingi tulipiga kura kwa
kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ukiachilia mbali kasoro
ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo.
Ndugu watanzania wenzetu, tangu juzi jumapili 25 Oktoba tulianza kupokea matokeo. Hiyo ni hatua muhimu sana kwa taifa letu, demokrasia yetu na amani ya nchi yetu. Wote tutakubaliana kwamba nchi nyingi za kiafrika zimeingia katika machafuko ya kisiasa na kuvuruga amani ya nchi hizo katika kipindi cha kupokea matokeo.
Nchi za Ivory Cost iliingia katika mgogoro wa kisiasa kwa wakati wa kupokea matokeo, ikaingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe maelfu ya wananchi walipoteza maisha, wengine wakijeruhiwa vibaya na wengi wakiyakimbia makazi yao.
Mwaka
2007, Nchi jirani ya kenya nayo ilingia katika mgogoro wa kupokea
matokeo na hivyo kusababisha machafuko, watu zaidi ya elfu moja walipoteza maisha, wengi wakiachwa walemavu na maelfu wakiyakimbia makazi yao.
Sisi
Global Peace Foundation Tanzania, tunaona mwenendo wa kupokea matokeo
ukianza kuingia dosari, kwa baadhi ya wagombea na wafuasi wa wagombea
kujitangazia matokeo. Ambao kwa Mujibu ka sheria ya uchaguzi ni kinyume,
ni kuvunja kanuni kwani chombo chenye dhamana ya kutangaza matokeo ni
Tume ya Taifa ya uchaguzi pekee.
Kwa
sababu hiyo, tumeona tuwakumbushe wanasiasa na viongozi wa vyama vya
siasa kuwa wakati huu wanapaswa kuwa watulivu na waangalifu pindi
wanapotoa matamko. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia wafuasi wao
kuwa watulivu na hatimaye kutuvusha katika hatua hii tukiwa na amani na
utulivu.
Tunaisihi tume ya uchaguzi ya Taifa NEC, na ile ya Zanzibar ZEC, kuharakisha mchakato wa kutangaza matokeo pindi yanapopatikana na kujumlishwa
ili kuepusha minong'ono na hisia hasi zinazoweza kupandikizwa kwa
wapiga kura na wananchi na baadaye kusababisha machafuko.
Tunakiri kuwa pamoja na kuwapo migogoro ya hapa na pale, kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika baadhi ya maeneo kama huko Unguja Zanzibar, baadhi ya maeneo ya Mbeya, Dar es Salaam na Lindi. Bado jeshi la polisi limeendelea kufanya kazi zake kwa weledi.
Hata hivyo tunakisii chombo hicho kuwa waangalifu zaidi katika kipindi hiki adhimu kwani matumizi ya nguvu zilizopitiliza yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani.
Hata hivyo tunakisii chombo hicho kuwa waangalifu zaidi katika kipindi hiki adhimu kwani matumizi ya nguvu zilizopitiliza yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani.
Tunawakumbusha watanzania wenzetu mashabiki wa vyama vya siasa , wapiga kura na vyama vya siasa wajiandae
kupokea matokeo ya aina yeyote. kwani misingi ya kidemokrasia inatutaka
kuchagua na yule aliyepata kura nyingi ndiyo anakuwa mshindi.
Na mwisho ni
kwa wanahabari na vyombo vya habari nyie mnabeba dhamana kubwa kwa
taifa hili katika wakati huu muhimu kwa taifa letu. Namna mtakavyotoa
taarifa kwa watanzania ndiyo itakayo amua mustakabali wa amani na
utulivu wa taifa hili. Mnalo jukumu na wajibu mahususi katika
kuhakikisha kuwa nchi hii inabaki salama, inabaki na umoja na
mshikamano, inabaki na utulivu. Toeni habari kwa kulingana na matakwa ya
taaluma yenu muhimu.
Waswahili husema, sindano ya daktari huponya na kuua na kalamu ya mwandishi hujenga ama kubomoa. Kama ilivyo daktari
mwema, mwenye maadili huchagua kuponya na mwandishi makini atachagua
kujenga jamii yenye amani, utulivu na mshikamano kwa kutambua kuwa bila
amani hakuna maendeleo.
Tunasimamia msemo wa watanzania uliopata umaarufu katika wakati huu wa uchaguzi kuwa KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI . Asanteni, Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania
Tafadhali bonyeza hapa chini kusikiliza wimbo maalumu wa kuhamasisha Amani ulioimbwa na Barnaba Boy
No comments:
Post a Comment