”Tamaa yangu na kwa kweli
jitihada za Serikali ya awamu ya Tano, zitakuwa katika ujenzi wa uchumi wa kipato cha kati ambapo
sura na maisha ya Watanzania walio wengi yafanane fanane na nchi ya kipato cha kati.
Njia moja ya kutufikisha huko ni uendelezaji wa
viwanda. ..... tutaanza na viwanda vilivyopo na kuha kikisha vinafanya
kazi.” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alipofungua rasmi Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dodoma, tarehe 20 Novemba 2015.
MCHANGO WA SEKTA YA VIWANDA,
BIASHARA NA UWEKEZAJI
Kwa kipindi cha 2005 hadi 2014,
ukuaji wa Sekta ya Viwanda umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 9.6 Mwaka 2005
na kufikia kilele cha asilimia 11.5 Mwaka 2007 kisha kuanza kushuka hadi
kufikia kiwango cha chini cha asilimia 4.1 Mwaka 2012 na kuanza kupanda tena
hadi kufikia asilimia 6.8. M waka 2014. Hivi sasa Pato la Taifa
linaongezeka zaidi (7%) ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda (5.2%)
Pamoja na ukuaji wa Sekta ya Viwanda
kuwa wa kupanda na kushuka, mchango wake katika Pato la Taifa kwa wastani
umekuwa ukiongezeka ijapokuwa katika kiwango kidogo (increasing at decreasing
rate). Aidha, mchango wa Sekta ya Viwanda
katika mauzo ya nje umefikia asilimia 23.31 Mwaka 2014 ikilinganishwa na
asilimia 9.31 Mwaka 2005(Jedwali Na 2)
Mheshimiwa Spika,
Idadi ya viwanda hapa nchini
imeendelea kuongezeka kutoka viwanda 125 Mwaka 1961 (wakati wa uhuru) hadi kufikia
viwanda 49,243 Mwaka 2013. Kasi kubwa ya kuongezeka viwanda imekuwa kati ya
Mwaka 2006 hadi 2013 ambapo vimeongezeka kutoka viwanda 5,153 Mwaka 2005 hadi viwanda
49,243 Mwaka 2013
.
Aidha, kati ya hivyo, viwanda vikubwa vinavyoajiri kuanzia watu 100 ni 247, viwanda vya kati vinavyoajiri kati ya watu 50 na 99 ni 170, viwanda vidogo vinavyoajiri kati ya watu 11watanona 49 ni 6,907 na vile viwanda vidogo sana vinavyoajiri chini ya watu watano ni 41,919.
Hiyo inadhihirisha kuwa, jitihada za Serikali
zinazoen delea kuelekezwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara
na kuendeleza viwanda vidogo, zitasaidia wananchi walio wengi zaidi kupata
ajira, kuongeza kipato na kupunguza masikini.
Vilevile, jitihada za
uhamasishaji zinazoendelea ufanywa na Serikali wa ushirikiana na SIDO, TIC, NDC
na EPZA ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vipya na kuongeza uwezo wa zalishaji
(capacity utilization) kwa viwanda vinavyozalisha chini ya uwezo uliosimikwa
(installed capacity) zitaongeza uzalishaji na idadi ya viwanda.
Chanzo: kalulunga Blogspot
Chanzo: kalulunga Blogspot
No comments:
Post a Comment