Mmoja wa Simba akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Baadhi ya Mamba wakiwa wamepumzika katika hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali.
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko.
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog
Hifadhi ya Taifa ya Katavi inapatikana kusini Magharibi mwa
Tanzania karibu na Ziwa Tanganyika katika Wilaya za Mpanda, Tanganyika na Mlele Mkoa wa Katavi inapatikana katika
latitude 6.63.7.34 kusini na na longitude 3.74.31.84 Mashariki.
Hifadhi hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1974 ikiwa
na ukubwa wa kilometa za mraba 2253 iliongezwa ukubwa mwaka
1996 na kufikia ukubwa wa kilometa za mraba 4471 na kuifanya kuwa
Hifadhi ya tatu kwa ukubwa Tanzania baada ya Ruaha na Serengeti .
Ilipata
jina lake kutokana na mzimu wa kabila la Wabende aliyejulikana
kwa jina la Katabi ambapo mpaka leo watu mbalimbali wamekuwa
wakifika ndani ya Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko
kwenye Ziwa Katavi wakiamini kuwa mzimu Katabi alikuwa akiishi
hapo zamani kabla ya kuwepo Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Jina
la Hifadhi hii lilijulikana kama Katabi kutokana na imani ya
jamii hizo kwa mzimu Katabi inaaminika kwamba mzimu Katabi una
uwezo wa kufanya miujiza ikiwemo kufanya mvua inyeshe , kuzuia
magonjwa ya mlipuko kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali.
Hifadhi
hii inafikika mwaka mzima kwa kupitia Mikoa ya Dar es salaam,Mwanza, Kigoma, Arusha hadi Mpanda kupitia Tabora kwa kutumia
usafiri wa ndege za kukodi "Chartered planes" au kwa njia ya
barabara kwa kupitia Mbeya na Sumbawanga pia kwa kutumia usafiri wa
Treni kutokea Tabora .
Hifadi ya taifa ya Katavi inawanyama wengi na adimu na wakubwa kuliko
wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi nyingine hapa Nchini
kutoka na hari ya uoto wa asili uliopo kwenye Hifadhi hii ambayo
kwa sasa imeanza kupata watalii tofauti na hapo awali .
Mbali
ya kuwepo kwa wanyama wengi madhari yake ni pana kuanzia
uwanda tambarare wa nyasi katika mkondo wa bonde la ufa hadi
kwenye miteremko mikali ambayo ni matawi mawili sambamba na bonde
la ufa la Mashariki maarufu kama bonde la ufa la Rukwa .
Uoto
uliopo unavutia unavutia sana kuanzia kuanzia Misitu iliyofunga
mpaka misitu ya wazi ,vichaka uwanda wa nyasi maziwa ya msimu ya
Chada na Katavi mabwawa na uoto kando ya mito.
Wakati
wa kipindi cha mvua kuna aina nyingi za maua aina ya 'species'
mbalimbali za miti na majani aina za 'species' 226 za miti zimeisha
tambuliwa zikiwemo aina tatu zenye mvuto wa kisayansi.
Uhai wa Hifadhi ya Katavi unategemea mto Katuma ambao
humwaga maji yake ziwa Katavi upande wa kaskazini ,Ziwa Chada
na mbuga yenye eneo la kilometa za mraba 425 ambayo hutuamisha
maji Floodplain katikati ya Hifadhi ziwa Chada hupokea pia maji
kutoka mto Kapapa ambao mkondo wake hutokea Kaskazini mwa
Hifadhi ya Taifa Katavi .
Kuna aina mbalimbali za wanyama pori ,idadi kubwa ya vipepeo
na ndege wa aina mbalimbali katika Hifadhi ya Katavi ni
kivutio vikubwa kwa wageni idadi ya watalii na shughuli za
maendeleo ndani ya Hifadhi bado ni ndogo hivyo kufanya
mazingira kuwa asilia zaidi .
Baadhi
ya wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi ya Katavi ni makundi
makubwa ya Tembo, Nyati, Simba, Pundamilia, Mbwa mwitu,
kongoni Swala paa, Nyemela na wanyama wengineo .
Pia
kwenye eneo la mto Stalike na Iku utakuta kuna makundi
makubwa sana ya viboko na mamba ambapo kumekuwa na mapigano ya
mara kwa mara na kufanya eneo hilo kuwa kivutio kikubwa kwa
watalii.
Upande
wa Hotel hifadhi hiyo inayo hotel nzuri za kufikia wagani ndani ya
Hifadhi iiingawa bado ni chache pia hotel nyingine
zinapatikana katika Kijiji cha Stalike ambacho kipo jirani na
Hifadhi na pia katika Mji wa Mpanda makao makuu ya Mkoa
wa Katavi uliopo umbali wa kilometa 40 kutoka Hifadhi ya Katavi.
Hivi
karibuni kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Elias
Manase aliwaambia wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wa
Mkoa wa Katavi kwamba Hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali.
Baadhi
ya changamoto hizo ni ujangili wa wanyama hasa Tembo ambao
unasababishwa na kuwepo kwa kambi za wakimbizi za Mishamo na
Katumba ambazo wanaishi Raia wa Burundi na Kongo.
Ilidai kuwa watu wanao ishi kwenye makazi hayo wamekuwa
wakiingiza silaha za kivita na kuziingiza nchini kisha wamekuwa
wakifanya ujangili wa kuuwa Tembo na kisha wanachukua meno ya Tembo
na kuyasafirisha kwenye soko la nchi jirani.
Changamoto
nyinginei ni uhaba wa miundo mbinu ndani ya Hifadhi kwani bado
haiku mizuri sana ingawa barabara zake zinapitika karibu mwaka
mzima.
Manase
alitowa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea Hifadhi
za Taifa kwani gharama ya kutembelea Hifadhi za Taifa ni ndogo
kuliko gharama ya mtu anayoitumia kwenye Bar kunywa pombe.
Askari
wa Hifadhi ya Katavi Joseph Mhina aliielezea Hifadhi ya
Katavi kuwa ni hifadhi ambayo ipo tofauti kabisa na
Hifadhi nyingine kwani watalii wanaotembelea Hifadhi hiyo huwa
wanawaona wanyama kiurahisi kabisa kwani watalii huwa ni wachache
hivyo huwa hakuna kugombania kuwaona wanyama kama Hifadhi
nyingine.
Chanzo:Katavi yetu Blog
No comments:
Post a Comment