Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 9, 2026

Mkuu Wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva Amechaguliwa Kuiwakilisha Tanzania Katika Programu Mahususi ya Uongozi Kwa Wanawake


Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva amechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika programu mahususi ya Uongozi kwa Wanawake inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf.

Programu hiyo inajulikana kama “Amujee Leadership Initiative” ikiwa chini ya Ellen Johnson Sirleaf Presidential Centre for Women and Development- EJS Centre inaungana na Wanawake Viongozi wengine waliopata fursa na heshima ya kushiriki.

Viongozi wengine ni Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Namibia, Dkt. Esperance Luvindao, Waziri wa Mazingira wa Guinea, Djami Diallo, Wabunge mbalimbali akiwemo Anta Diack wa Senegal na Dkt. Anneline Chetty ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Biashara, Viwanda na Uwekezaji Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa, Victoria ni miongoni mwa Wanawake 15 walioteuliwa barani Afrika baada ya mchujo mkali uliovutia zaidi ya waombaji 600. Uteuzi wake umetokana na mchango wake katika Uongozi wa Jamii, hususan kazi za maendeleo Vijijini na uwezeshaji wa Vijana kupitia nafasi yake ya Uongozi wa Wilaya.

Programu hii inalenga kukuza ushirikiano wa Viongozi Wanawake barani Afrika na kuimarisha ajenda za maendeleo jumuishi, huku ikitarajiwa kuongeza fursa za ushirikiano kati ya Mataifa ya Afrika.

No comments:

Post a Comment