Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, July 28, 2012

HUU HAPA MPANGO MZIMA WA TAMASHA LA WACHAGGA LEADERS CLUB...!

 

Mkurugenzi wa My Way Entertainment Paul Maganga akiongea na waandishi wa Habari katika Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam Jana.

BENDI  zenye ushindani mkubwa na mashabiki wengi nchini za African Stars 'Twanga Pepeta' na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
 

Akizungumza na waandishi wa habari  mapema jana katika ukumbi wa Idara ya  Habari Maelezo, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga walioandaa tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya SBC Tanzania Limited, kupitia kinywaji cha Pepsi, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambao watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakila na vinywaji vya asili kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa  tamaduni zao  yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro,  SBC Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata Decorations.

No comments:

Post a Comment