Eric Shigongo (kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
MD wa Global
Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema leo ameongea na media kuhusu madai
ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye jana alikwenda Ubalozi wa
Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza kurejeshewa paspoti yake.
Eric amefunguka
kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya
kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja
wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii
huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili
kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo yalikubaliwa.
Mazungumzo hayo
ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agenti wa Chameleone
ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake
ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa kweli anawasilina na
kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli.
“Tulipokubaliana
nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha,
ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George
na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba
yetu”, alisema Shigongo.
Akielezea zaidi,
Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George
pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na
kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo
fedha.
“Chameleone
alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea advace ya dola
3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo
wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.
“Baadae Jose
alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti wake, kitu ambacho
kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na ajenti wake
kwetu sisi.
“Kwa kuwa ujio
wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers,
ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana
kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya
kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege.
“Ndugu zangu,
sikua na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu
tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa
barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa
uchungu.
Hivyo mara baada
ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake kwenda mpaka
Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia dola 8000 na
kusaini mkataba mwingine wa pili.
“Ni dhahairi
kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa kushirikiana na
ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye tumeshafanya naye kazi
mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni Chameleone ndiye
aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo ulikuwa ni mchezo
wa pamoja, na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani ameshawafanyia
mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini Kenya.
“Dola 3,500 siyo
fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa
ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya
upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,”
alihoji Shigongo.
Mwisho Shigongo
alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala hili, kwani Chameleone
ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini
Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya na kubamiza mlango,
akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote wapatao miloni 40!
No comments:
Post a Comment