Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 31, 2012

John Mnyika: Sekta ya afya taifa linarudi nyuma kwa ari, nguvu na kasi zaidi; Tuungane kumshauri Rais...!

John Mnyika
Kwa Sekta ya afya taifa linarudi nyuma kwa ari, nguvu na kasi zaidi; tuungane kumshauri Rais kuingilia kati kuwezesha wigo wa mapato kupanuliwa kupitia marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha na hatimaye tuletewe bajeti ya nyongeza kwa ajili ya sekta ya afya tupunguze upungufu wa madawa, vifaa tiba na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma kwenye sekta ya afya wakiwemo madaktari. Bajeti iliyopitishwa leo utegemezi wa fedha za nje kwenye fedha za maendeleo umeongezeka na kufikia asilimia 93 kwa bajeti ya 2012/2013 wakati kwa mwaka 2011/2012 wahisani walitimiza ahadi zao kwa asilimia 36 tu pamoja na kuahidi zaidi ya asilimia 90. Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 imeshuka mpaka asilimia 10.4 tu ya bajeti ya Serikali wakati wastani kwa miaka sita mfululizo nimepiga mahesabu ilikuwa ni asilimia 11. Serikali imekiri bungeni kuwa kiwango cha bajeti kinachotengwa kwenye sekta ya afya kinapungua badala ya kuongezeka kufikia asilimia 15 ambayo iliridhiwa Abuja mwaka 2001 zaidi ya miaka 10 iliyopita. Kilichonisikitisha zaidi ni kuwa Waziri amesema kuwa Rais atahakikisha lengo hilo linafikiwa ifikapo 2015. Tujadili kwenye bunge la wananchi na kuchukua hatua, Maslahi ya Umma KWANZA

No comments:

Post a Comment