Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, July 7, 2012

MAMA KANUMBA ATEGA MAMILIONI...!

Flora Mtegoa.
Stori: Gladness Mallya
MAMA mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ameyatega mamilioni ya fedha kwa kufungua banda katika Maonesho ya Sabasaba linalomhusu mwanaye.
Katika banda hilo, mama huyo ameweka vitu mbalimbali vya marehemu Kanumba vikiwemo nguo, viatu, miwani, gitaa na kinanda, lengo likiwa ni kuwapa nafasi mashabiki wake kuviona na kununua bidhaa zenye picha ya mwanaye kama vile vikombe, fulana, ‘key holder’ na nyinginezo.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya watu waliokutwa kwenye banda hilo wamempongeza mama huyo kwa ‘idea’ hiyo kwani licha ya kwamba huenda ikamuingizia fedha nyingi lakini pia amewapa nafasi mashabiki wa marehemu kuviona vitu vyake.
“Ni wazo zuri kwa kweli na hapa anaweza kujiingizia mamilioni ya fedha kwani marehemu ana mashabiki wengi hivyo ni lazima watatembelea kwenye banda hili,” alisema Sessy Salawa wa Ilala.
Akizungumza na mwandishi wetu kwenye banda hilo, mama Kanumba alisema: “Hapa kuna vitu vya Kanumba vya maonesho ambavyo siviuzi ila kuna fulana, vikombe na bidhaa nyingine zenye picha ya Kanumba ambavyo naviuza, watu waje kwa wingi kujionea,” alisema mama huyo.

No comments:

Post a Comment