Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 31, 2012

WASHINDI WA VODACOM WA TUZO ZA UMAHIRI WA DIGITALI...!


 
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza na kuwakabidhi washindi wa Tuzo za umahili wa digitali za Vodacom Tanzania,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Bi.Joseline Kamuhanda,kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya aimgroup iliyoendesha zoezi zima la kuwapata washindi hao Bw.Nadeem Juma.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imetangaza washindi wa Tuzo za Umahili wa Digitali za Vodacom, katika kipengele cha mitandao ya jamii na tovuti.
Tuzo hizi ni katika mpango wa Vodacom kutambua, kuendeleza na kuongeza jitihada na maudhui katika mitandao ya kijamii na tovuti na kuthamini mchango wa waandishi katika utoaji wa taarifa kwa jamii.
Washindi wamepatikana kutokana na mchujo uliofanywa na majaji wenye weledi katika maswala ya mitandao. Washindi wamepatikana kutokana na vigezo mbalimbali kwa jumla ya alama 360 ambazo zitatolewa katika wavuti ya mashindano.
Washindi kumi walioshinda katika kipengele cha Mitandao ya jamii na tovuti ni:
-          Elsie Eyakuze wa Mikocheni Report, kwa jitihada zake katika kutoa maoni na kukosoa masuala mbalimbali kwa uchambuzi makini.
-          Muhidin Michuzi wa Issa Michuzi, kwa kuwa mwanzilishi wa kwanza katika mitandao ya jamii na kutoa hamasa kwa watu wengine.
-          John Kitime wa Wanamuziki Tanzania kwa kuhakikisha kuwa wanamuziki chipukizi wa Tanzania wanajifunza kutoka kwa wasanii nguli waliopita.
-          Masoud Kipanya wa Kipanya.co.tz kwa jitihada zake katika kutumia vyombo mbalimbali katika kutoa taarifa za kijamii na kisiasa kupitia vibonzo ( katuni)
-          Umoja wa Vijana FM wa Vijana FM kwa kuonyesha ushirikiano, uchambuzi na kutoa elimu kwa jamii katika masuala ya Digitali.
-          Millard Ayo wa Millardayo.com kwa kutumia umashuhuri wa radio yake kuwataarufu wasikilizaji na mashabiki katika masuala mbalimbali ya kitamaduni Tanzania.
-          Miriam Rose Kinunda wa Taste of Tanzania kwa kuonyesha dunia undani wa utamaduni wa kiswahili kwa moyo na bila kuchoka.
-          Mike Mushi wa Jamii Forums, kwa kutoa fursa kwa watu kujadili na kuchangia masuala mbalimbali kwa uwazi.
-          Rachel Hamada wa Mambo Magazine kwa kufungua milango kwa Tanzania na kuwavutia watu wengine wa sehemu tofauti duniani.
-          Fatima Hassan wa DJ Fetty Blog kwa kuonyesha upendo wake katika muziki na utamaduni na kuwashirikiana na Watanzania.
Washindi waliotajwa hapo juu ni katika kuwawakilisha wachache kati ya wengi wanaoonyesha vipaji vyao ambao pia mchango wao unahitaji kuthaminiwa.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Bw. Kevin Twissa amesema kuwa washindi hao ni wale ambao kweli wanaongoza katika tathnia hiyo na wataendelea kuwa na mafanikio makubwa zaidi siku za usoni.
“Kwa heshima kubwa tunawapongeza washindi wote katika Tuzo hizi za umahili wa digitali katika kipengele cha mitandao ya jamii na tovuti,” amesema na kuongeza kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutambua na kuthamini michango ya waandishi wa mitandao ya jamii na tovuti katika kuleta mabadiliko kwa watanzania.

Read more: VODACOM YATANGAZA WASHINDI WA TUZO ZA UMAHIRI WA DIGITALI - BongoCelebrity

No comments:

Post a Comment