Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 11, 2012

AJALI NYINGINE TENA YATOKEA MOROGORO LEO...!



Basi la kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es Salaam na Mwanza likiwa limeacha njia na kupinduka baada ya kutokea ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro

Mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi la Shabiby, Deogratias Mrai akiwa katika wodi namba moja ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro akiuguza majeraha aliyopata kufuatia basi hilo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika eneo la Mkundi-Makunganya Manispaa ya Morogoro lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa.


Ajali hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi kwa kuhusisha mabasi matatu, Kampuni ya Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, Allys Sport na Sumry yaliyokuwa yakitokea Morogoro kwenda Mwanza.
Baadhi ya majeruhi waliokuwa wakisafiri na basi la Shabiby walisema basi hilo lilianza kuyumba na baadaye kuacha njia kisha kupinduka.

Mmoja wa abiria hao, Rashid Shaaban alisema baada ya basi hilo kupinduka, ghafla waliona basi jingine la Sumry likiacha njia na kupinduka wakati lilipojaribu kulipita gari jingine jirani na eneo hilo.

Alisema kuwa wakati kukiwa na msongamano wa magari katika eneo hilo la ajali, basi jingine la Allys Sport liliacha njia na kupinduka na hivyo kutokea ajali tatu katika muda usiozidi dakika 10.

Shaaban alisema baada ya ajali hizo walitokea watu waliokuwa wakijifanya kutaka kutoa msaada, lakini lengo lao lilikuwa ni kuiba mali za majeruhi. Hata hivyo, alisema lengo lao hilo halikufanikiwa kwani muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hizo, askari walifika na kuimarisha ulinzi.

Sourse: Juma Mtanda

No comments:

Post a Comment