Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 15, 2012

BIBI HARUSI AMUUA MUME WAKE MUDA MCHACHE KABLA YA KUFUNGA NDOA...!

Katika hali ambayo haikutarajiwa, mwanamke mmoja wa nchini Marekani
amemuua kwa kumpiga kisu cha moyo mchumba wake katika siku ya harusi
ambayo wangefalishana pete za pingu ya maisha pamoja.

Wakati maandalizi ya harusi yakiwa kwenye hatua za mwisho, watu wakijiandaa
kwenda kanisani, bi harusi alimuua bwana harusi kwa kumchoma kisu
kilichoutoboa moyo wake.

Polisi wa Pennsylvania waliukuta mwili wa bwana harusi, Billy Rafeal Brewster
ukiwa nje ya nyumba yao ikiwa ni masaa machache kabla ya harusi kufungwa.
Bwana harusi alifariki ndani ya lisaa limoja baada ya kufikishwa hospitali.

Bi Harusi aliyejulikana kwa jina la Na Cola Darcel Franklin alitiwa mbaroni na
alipandishwa kizimbani siku hiyo hiyo kwa mashtaka ya mauaji.

Na Cola huku akionyesha huzuni na mshangao mkubwa alimtaka jaji aruhusu
watu waangalie tena hali ya mumewe mtarajiwa kwani hakuamini kama ni kweli
mchumba wake amefariki.

Huku akibubujikwa na machozi, Na Cola aliiambia mahakama kuwa hakumuua
mpenzi wake kwa makusudi na alitaka aruhusiwe aondoke arudi kwake akaonane
na familia yake.

Taarifa zilizopatikana zilieleza kuwa siku ya tukio hilo jumamosi asubuhi, bwana
harusi aliwaambia wageni waliokuja kwenye harusi yake waliofikia nyumbani
kwake kuwa anatoka nje kwenda kuwanunulia chakula.

Mzozo uliibuka kati yake na bi harusi na ndipo bi harusi alikimbilia kisu na
kumchoma bwana harusi mara mbili kifuani.

Polisi walithibitisha kuwa uchunguzi wa maiti umeonyesha kuwa shambulio hilo la
kisu liliutoboa moyo wa bwana harusi na kupelekea kifo chake.

Taarifa zaidi zimeongeza kuwa mchungaji aliyekuwa afungishe ndoa hiyo na
baadhi ya watu waliowasili kanisani kwaajili ya harusi hiyo iliyopangwa kufanyika

saa nne asubuhi walilazimika kwenda nyumbani kwa bwana harusi kujua kwa nini
hawakuja kanisani kufunga ndoa.

Huko ndipo walipokutana na taarifa kuwa bwana harusi ameuliwa na bi harusi.

No comments:

Post a Comment