Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 15, 2012

WANAWAKE WAAMUA KUJENGA MJI WAO WENYEWE NA HAWATA RUHUSU MWANAUME KUINGIA KWENYE MJI HUO...!

Kwa mara ya kwanza duniani, mji ambao wanaume hawataruhusiwa kuishi
unajengwa nchini Saudi Arabia ambapo ni wanawake pekee watakuwa
wakiruhusiwa kuishi na kufanya kazi kwenye mji mpya utakaojengwa kisasa.

Mji mpya kwaajili ya wanawake pekee ukiwa na viwanda mbalimbali unajengwa
nchini Saudia Arabia ambapo katika mji mzima wanawake wataishi wenyewe na
wakifanya kazi bila ya kuwepo ya hata mwanaume mmoja.

Katika kuwapa nafasi wanawake kufanya kazi kwa uhuru kama wanawake wa
sehemu zingine duniani, Saudi Arabia inatarajia kujenga mji wa kisasa kwaajili ya
wanawake pekee.

Mji huo utakaogharimu dola za Marekani milioni 133 utaanza kujengwa
mwanzoni mwa mwakani karibu na mji wa mashariki mwa Saudi Arabia wa Hafuf.

Mji huo utakuwa na viwanda vya nguo, madawa na vyakula na inakadiriwa kuwa
jumla ya wanawake 5,000 watapata ajira.

Hatua hii ya kuanzishwa kwa mji wa wanawake pekee inakuja ili kuwapa nafasi
wanawake kuendana na wakati na kufanya kazi na pia kuwapa mazingira ya kazi
yatakayoenda sambamba na sharia za kiislamu.

Mamlaka ya viwanda ya Saudia, Modon imesema kuwa ina mpango wa kuanzisha
mji wa pili wa wanawake pekee mbali na mji wa Hafuf.

No comments:

Post a Comment