Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 3, 2012

HALI TETE YAIBUKA GWATA...!

Kijiji cha Gwata Wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani umeingia doa jingine baada ya
vita kali kuibuka kati ya wafugaji na wakulima. Katika tukio la hivi karibuni majira ya asubuhi wafugaji wa jamii ya kimang’ati waliwashambulia ndugu
wa familia ya bwana bwengo, ambapo watoto wa bwana bwengo,Hamis Bwengo na
Said Bwengo walifanyiwa unyama kutoka kwa watoto wa Bepodo tajiri kutoka jamii ya
kimang’ati ambapo watoto hao wa mfugaji huyo walipowapiga bila huruma watoto hao
wa mkulima Bwengo. Baada ya habari za kupigwa kwa wakulima hao taarifa zilifika
kijijini hapo na Afisa Mtendaji alishinikizwa kuita mgambo ili kwenda kuwakamata
watuhumiwa hao. Kazi nzuri iliyofanya na mgambo hao ilifanikisha kukamatwa
kwa watuhumiwa hao na kuamuliwa wapelekwe wilayani kwa ajiri ya kufunguliwa
mashitaka.

Safari ya kuwapeleka majeruhi hospitali ilifanyika sambamba na watuhumiwa hao
kupelekwa kituo cha polisi.

Katika hali ya kushangaza siku iliyofuata watuhumiwa hao walionekana mitaani
kijijini hapo huku wakijisifu kwa kusema Serikali ipo mikononi mwao na hakuna
wa kuwasumbua Huku hali za majeruhi zikiwa si za kuridhisha. Tajiri Bepodo
anayesadikiwa ana ng’ombe zaidi ya elfu mbili amekuwa mtu wa kujigamba na kukebehi
hatua ya wao kupelekwa polisi kwa madai kuwa ana watu wake.

Hii imejitokeza ikiwa wakazi wa gwata wakiwa hawajasahau tukio la hivi karibuni,
Ambapo wakulima wengine walipopigwa na wafugaji wa jamii hiyohiyo ya kimanga’ati
na hata walipokamatwa na kufikishwa kituoni dakika chache waliachiwa na walirudi
kijijini na washitaka wao tena ndani ya basi moja.

Hali ya uongozi wa Kijiji cha Gwata ikiendelea hivi, inaweza kusababisha vita kali kati
ya wafugaji na wakulima. HII Inatokana na malalamiko ya wakulima kutokufanyiwa
kazi.

Malalamiko mengi yanamuangukia Afisa Mtendaji anayehusishwa na tuhuma za rushwa
kutoka kwa wafugaji, malalamiko mengine ni kuhusishwa uporaji wa mashamba ya
wakulima. Na kugawa bila kufuata utaratibu.

Wakazi wa maeneo ya Gwata wenye mapenzi mema na Gwata na Tanzania wanaomba
kwa WAZIRI WA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA na Idara
zinazohusika, Kutatuliwa kwa kumuondoa mtendaji huyo na hatua kali zichukuliwe
kwani ameshindwa kutimiza wajibu wake na kazi na kupelekea uhalibifu wa mazao, na
migogoro ya mara kwa mara kati ya wafugaji anaowalinda na wakulima aliowatenga.
Anachangia kuweka matabaka kati ya wenyeji(wazaramo) na wageni kutoka nje ya mkoa
wa Pwani. Mkuu wa Mkoa na Wilaya wameshughulikia bila mafanikio.

No comments:

Post a Comment