Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 29, 2012

HAYA NDIO MAELEZO YA T.I.D KUHUSU TAARIFA ZA KUTAKA KUMUUA ALLY KIBA...!

Kushoto ni Ally Kiba na T.I.D

Chanzo chetu kimeripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa saa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa saa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa na Chanzo chetu, T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
Chanzo chetu kilipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibu kwa kusema “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi  lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”

Kwa taarifa zaidi kuhusu sakata hili endelea kutembelea mtandao wetu wa www.kingjofa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment