Huu ni umati wa watu kutoka maeneo mbalimbali walivyofurika kwenye Tamasha la Dini
lililopewa jina la LOVE TANZANIA linaloendelea katika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es Salaam likiongozwa na Askofu Andrew Palau kutoka
Marekani.
Vijana walioongoza na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na mafundisho ya dini kwa njia muziki.
Wana Dar es Salaam wakiendelea kumiminika katika viwanja vya Jangwani.
Mmoja wa Wahudumu katika Tamasha hilo akipata chakula cha mchana na familia yake Uwanjani hapo.
Umati wa watu ukiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya chakula uwanjani hapo.
Moja ya
Magari na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi iliyopewa Zabuni ya kusafisha
Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd likiwa limepaki katika Viwanja
vya Jangwani kuhakikisha Usafi unazingatiwa Uwanjani hapo wakati tamasha
la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiendelea.
Pichani Juu
na Chini ni moja ya michezo iliyofanyika kama sehemu ya burudani
uwanjani hapo ambapo ilionekana kuvutia Umati wa Watanzania
waliohudhuria tamasha hilo.
Vijana, Watoto kwa Wazee wakitazama mchezo wa mapikipiki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd akihakikisha swala usafi linazingitiwa uwanjani hapo kama inavyoonekana.
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia mchezo wa Baiskeli.
Palikuwa hapatoshi Jangwani.
Ulinzi na Usalama kwa raia ulikuwepo.
Familia zikiendelea kula, kunywa na kufurahi uwanjani hapo.
Hili ni
Jukwaa la kimataifa kutoka nchini Uganda maalum kwa ajili ya Tamasha
lililopewa jina la "LOVE TANZANIA" likiongozwa na Askofu Andrew Palau
kutoka nchini Marekani, haijawahi kutokea kusikia Sound na Mziki wa
Ukweli nchini kwa mliohudhuria tamasha hili mtasema.
No comments:
Post a Comment