Wajukuu wa marehemu mzee Roman Selasini wakitoka kanisani wakielekea nyumbani kwa mzee Roman kuendelea na taratibu za mazishi ya babu yao.. .
Mwili wa marehemu Mzee Roman Selasini Shao ukiwa kwenye jeneza na pembeni ni mtoto wake wa kiume.
Mtoto wa Marehemu mzee Roman wakiwa eneo alipozikiwa baba yao.
Hawa ni kati ya Viongozi wa kisiasa waliohudhuria kwenye msiba wa mzee Roman Selasini.
Ikiwa ni miezi miwili imepita toka afariki mke wa Mzee Romani Selasini Shao ambaye ni baba yake na Mbunge wa jimbo la Rombo. Leo ndio yalikuwa maziko ya Mzee Roman Selestini Shao aliyezaliwa mwaka 1922, na katika kipindi cha uhai wake alipata kushika vyeo mbalimbali serikalini na cheo alichoweza kudumu nacho kwa muda mrefu ni cheo cha udiwani kupitia chama cha CCM kata ya mikiidi wilayani Rombo, Mzee Roman Selasini Shao alikuwa diwani tokea mwaka 1972 hadi mauti yalipo mkuta, licha ya cheo hicho pia aliwai kuwa mwalimu wa shule ya msingi na baadae akawa mwalimu wa shule ya sekondari, pia aliwai kuwa afisa elimu wa wilaya ya Rombo na baadae akawa afisa elimu katika mikoa tofauti tofauti hapa Tanzania. Pia alikuwa mwenyekiti wa shule ya sekondari mikiidi na na mjumbe wa bodi ya shule ya sekondari mkuu, na si vyeo hivyo tu pia alikuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Rombo. Marehemu alikuwa na watoto 14 wajukuu 40 na vitukuu 6.
Team nzima ya KILIMANJARO OFFICIAL BLOG inawapa pole sana ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu..
No comments:
Post a Comment