Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 31, 2012

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wahamiaji haramu 24...!

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wahamiaji haramu 24 ambao walikuwa wakihifadhiwa katika nyumba ya mkazi mmoja katika kijiji cha Jipe wilayani Mwanga.
Akizungumza na chanzo chetu makini, kaimu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Costantine Maganga amesema kuwa wahamiaji hao wameingia nchini agusti 30
mwaka huu na kuhifadhiwa nyumbani kwa Bwana Yasin Mrutu.

Amesema raia hao wametokea nchini Ethiopia  na kufika nchini kinyemela, kwa lengo la kuelekea Afrika ya kusini  kwa kupitia nchini Zambia.
Kamanda Maganga ameongeza kuwa juhudi za wananchi wa wilaya hiyo za kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ndizo zilizofanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu.

Aidha amewataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ilikusaidia na kufanikisha utendaji kazi wa jeshi hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likifanya kazi kwa karibu kabisa na wanajamii.

No comments:

Post a Comment